Vitu Vidogo Vina Maana Kubwa Sana: Vitu Arobaini Na Nne (44) Vitakavyoyafanya Maisha Yako Kuwa Bora.
kiwa unataka kuishi maisha yenye furaha, afya tele na yenye mafanikio ni lazima kukusudia kuhusu kufanya vitu vidogo vitakavyoweza kuyafanya maisha yako kuwa bora. Kuboresha maisha yako ni kuhusu kufanya vitu vidogo vitakavyoambaa na safari yako na kuweza kukuletea furaha, afya na mafanikio ndani ya maisha yako. Kuna vitu vidogo unavyohitaji kuvifanya ili uweze kuwa bora ,vitu hivyo vidogo vina maana kubwa sana katika maisha yako. Vitu hivyo vitakusaidia kuwa mtu unayetaka kuwa ili kuweza kuyafanikisha malengo yako pamoja na kuishi maisha unayotaka kuishi. Vifuatavyo ni vitu Arobaini na nne (44 unavyohitaji kuvifanya ili kuyafanya maisha yako kuwa bora.
1. Twaa mtizamo chanya; Muone kila mtu na kila kitu kama msaada mkubwa kwako. kutazama kwa njia hii kunaweza kujenga muujiza mkubwa katika maisha yako. Mshukuru kila mtu na kila kitu na uvione kuwa ni msaada mkubwa kwako na utaweza kuboresha mahusiano yako na kuweza kuwa bora zaidi.
2. Jihatarishe; fanya kitu fulani nje ya eneo lako la faraja( comfort zone). kama vile kuzungumza na mtu fulani aliye nje ya mzunguko wako wa kijamii katika sherehe wakati ambao unakuwa ni mwenye aibu au mwenye kuona haya. Kujitolea kumsaidia mtu fulani katika kukamilisha mradi ambao utahitaji ujuzi mpya katika kazi. Kwa kufanya hivyo utapanua upeo wako, mawazo yako kuhusu wewe ni nani na nini unachoweza kukifanya.
3. Kubaliana na hiari; fanya kitu fulani kwa hiari. kama vile kwenda kwenye mgahawa ambao hujawahi kwenda, kuamka mapema asubuhi ili tu kutumia dakika chache katika kuzungumza na mtu fulani kabla hajakwenda kazini, kutoa salamu kwa mtu yeyote mpya. Vitu hivyo vidogo, ijapokuwa havina maana yoyote, vinaweza kuwa na matokeo ya kushangaza, matokeo ambayo yataweza kubadilisha maisha yako na kuwa bora.
4. ione kwanza kabla ya kuwa nayo; tumia nguvu ya maono katika kuchochea maisha yako ya baadaye. Mara nyingi, huwa tunaishi maisha yetu bila ya kufikiri kuhusiana na kesho yetu. Ni muhimu ukatenga muda kila siku na ujipe taswira au upige picha akilini mwako jinsi unavyotaka kuwa na maisha utakayokuwa unaishi baada ya miaka mitano au kumi ijayo. Jione utakuwa wapi na utakuwa unafanya nini na maisha yako yatakuwa vipi. Unaweza ukapiga hatua kwa urahisi zaidi kuelekea kwenye ndoto zako ikiwa tu utaanza kuwa na picha sahihi akilini mwako juu ya kule unapokwenda au kutaka kupafikia( kuwa na maono).
5. Onyesha upendo wako katika njia zisizotarajiwa; fanya kitu kidogo kwa ajiri ya mume au mke wako kila wiki. Hii inaweza kuwa kama vile kumwandika mume au mke wako ujumbe wa upendo, au kwa kununuliana kitu chochote kile kilicho kizuri. Usiwe mbinafsi, hivi ni vitu vidogo sana kuvifanya lakini vinaweza kujenga ndoa nzuri pia.
6. Tazama yaliyo bora katika watu; Jipe ahadi ya kutoa pongezi au sifa kila siku kwa watu wasiopungua kumi. Toa sifa zako au pongezi zako kwa kila mtu, kama kuna mtu atakuwa amevaa na amependeza vizuri mpe sifa zake, awe amefanikisha jambo fulani mpe pongezi au msifie.
7. Vunja ukimya; tabasamu, toa salamu ,sema hujambo, na shirikiana na kila mtu unayekutana naye. Uhusiano wako chanya na ulio halisi pamoja na wengine utafundisha ukuu kwa mfano, na juhudi zako sio tu zitamwinua mtu mwingine, na utashinda aina zote za marafiki wapya.
8. Tafuta njia ya kuwa mkarimu kwa watu; Kuwa mkarimu kila siku. Fungua mlango na utoe neno“ nakupenda” kwa mtu yoyote yule ambaye hamjaonana kwa muda mrefu sasa. Wasaidie wazee kwa kuwabebea mizigo na kuwapisha kwenye viti n.k. ikiwa utazingatia makini majibu yao ,utaweza kuing’arisha siku yako na kuifanya kuwa siku nzuri.
9. Zingatia maoni ya wengine kuliko yako; Ikiwa utawahukumu watu, utakuwa hauna muda wa kuwapenda; kwa hiyo, usijaribu kuwahukumu au kufanya mapendekezo na mawazo yako mpaka pale utakapoijua hadithi yote. Kuwa na shukrani kwa kila mtu unayemjua. Watu ndio ni rasilimali au mali iliyo kubwa kwetu. kwa hiyo, kuwa mkarimu kwa kila mtu. Chochote tutakachokipanda ndicho tutakacho vuna. Kama tutapanda mbegu za imani kwetu binafsi na kwa wengine ,tutaweza kuvuna na kupokea wingi wa marafiki waaminifu katika maisha yetu.
10. Sambaza furaha; tabasamu kwa kila mtu, kwako binafsi pale unapojiangalia katika kioo, toa tabasamu kwa bosi wako, familia yako, mpita njia, mfanyakazi mwenzako, muuza duka, karani. Tabasamu, kwa sababu tu, Kutabasamu kunajenga urafiki, kukubaliwa, kueleweka, na pia kuna burudisha .
11. Mahusiano bora; Kuwa karibu na familia yako (vizazi vyote) na rafiki zako. Hawa ni watu wenye maana kubwa sana kwako, na watakufuata kupitia maisha. Usiviache vitu vipate kukaa katika njia ya mahusiano yako na watu
12. Jifunze kitu kipya leo; Bakia wazi katika kujifunza, kuwa mtu anayekubali ukuaji na mabadiliko. Kuna kitu kipya cha kujifunza kila siku. Kutoka kwenye ufahamu au uzoefu wako, kutoka kwa mtu unayemjua, kwenye vitabu, semina, mtoto wako, wazazi wako. Bakia wazi. Maisha ni kuhusu kukua na kujifunza. Ukuaji na mabadiliko kunatuletea maisha, kadri tunavyozidi kujifunza zaidi, ndivyo tutakavyozidi kuwa hai zaidi. Na kumbuka akili yako ni sawa na mwamvuli, huwa inafanya kazi vizuri pale inapokuwa wazi.
13. Sikiliza kuelewa; Ili kuweza kuyafanya maisha yako kuwa bora sasa, bakia na mawazo yako. Sio muhimu ukubaliane au usikubaliane na mwingine, lakini sikiliza kwa makini. Kuruhusu wengine wakwambie kunaweza kusafisha njia kwa urafiki wa baadaye. Na kwa kiasi kikubwa kutakupatia imani ya mwingine na utapa mshirika pale atakapohitajika.
14. Waheshimu wanaofanya maisha yako kuwa rahisi; Kuwa mkarimu na mwenye heshima, hasa kwa wafanyakazi wale wanaotoa huduma. Wao pia wanatengeneza pesa zao kama alivyo kila mtu.
15. Wajibika kwa mawasiliano yako; Wakati ambao unapata majibu usiyoyatarajia .Usimlaumu mtu yeyote. badili maneno yako na hali ya nia yako na ujaribu tena mpaka pale utakapo weza kupata matokeo na majibu unayoyataka. Utapata urafiki wenye nguvu. Kwa hiyo, kutokukubaliwa au kutokubaliana kunaweza kutatuliwa kwa kuitwaa imani ya aina hiyo. Wajibika kwa mawasiliano yako.
16. Wafanye wengine wajisikie kukaribishwa; Popote utakapo kuwepo hakikisha watu walio karibu nawe wanajisikia kukaribishwa na kushirikishwa. Hakuna hata mmoja anayetaka kujisikia kuachwa au kutengwa katika kila jambo.
17. Wakubali watu; Epuka kujiumiza au kukata tamaa na kujiletea huzuni. Wakubali watu kwa jinsi walivyo, na pale walipo katika maisha na wala sio unapotaka wewe wawe au unavyotaka wawe wanafanya nini.
18. Sherekea; ionyeshe akili yako, mwili wako na roho yako kuwa kusubiria kote, jitihada zote ulizozifanya, kung’ang’ania kote pamoja na kuvumilia kote kuwa kunalipa na kumekulipa. Sherekea kwa mafanikio uliyoweza kuyafanikisha.
19. Acha asili iinue roho yako; Kuchukua dakika kumi na tano(15) katika wakati wa kazi zako na kisha kutoka nje na kutazama kwa karibu. kaa mahali fulani na ujionee asili. Tazama kwa karibu sana kwenye maua ,mawingu, pumua na weka zaidi umakini wako. Na mwisho wa pumziko lako utajisikia kuwa mtulivu, kuburudishwa na kutaka kuthamini zaidi asili n.k. Kuna matokeo makubwa katika kufanya hivyo.
20. Kuwa mkweli kwako mwenyewe; Kuwa mkweli kwako mwenyewe, badala ya kuzizimua nguvu zako kwa kujaribu kujilinganisha au kujifanya kuwa mtu fulani ambaye siye wewe. Tambua na kisha ugawe mkusanyiko wako wa kipekee wenye ubora, ufahamu, ujuzi na vipaji vyako ambavyo ni wewe peke yake ndiye utakayeweza kuvichangia katika dunia hii. Usijiringanishe na wengine.
21. Onyesha kuthamini kwako; Usimwache mtu asionekane, kuna watu fulani wanatumia maisha yao katika kutaka kuonekana, kufahamika, kusikika, kukubaliwa na kuthaminiwa. Wakati mwingine huwa inachukua dakika tano (5) tu kuifanya siku ya mtu kama huyo au mtu fulani kuwa nzuri. Kama vile kumjulia hali mtu , kupata kujua familia yake inaendeleaje n.k. Usijaribu kumwacha mtu akienda au akiondoka bila ya kumsimamisha na kuonyesha mvuto katika yeye.
22. Usiwe mbinafsi; Toa neno ”mimi” katika misamiati yako na uangalie jinsi maisha yatakavyo kuzawadia. Kama tabia yako inafafanuliwa sana na kile unachokifanya kwa ajiri yako, basi inakuwa inakosa thamani yoyote na wala haina maana yoyote au haifai kabisa .Acha maisha unayopumua ndani ya wengine yafafanue tabia yako, na uangalie maisha yako yakiongezeka.
23. Weka viwango vyako juu; Chora mstari kisha ishi juu yake ,mambo mengi yaliyohasi unayokutana nayo katika maisha huwa yanaanguka sana chini ya mstari; shaka, hofu, kujiuzulu pamoja na kushindwa. Lakini furaha, shukrani, imani, uaminifu huwa vinainuka juu yake. Pambana kuishi juu ya mstari rafiki.
24. Ishi maisha yenye matunda; Ona kila changamoto unayokumbana nayo kama fursa ya kukua. Vitu Fulani katika maisha vinaweza kutufanya kuwa bora au wenye uchungu, chagua kuishi maisha yako kwa kutumia masomo muhimu yanayosababisha ukomavu wa kihisia au kuimarisha tabia yako. Pambano kubwa katika maisha yetu lipo akilini mwetu. Kwa hiyo, tunahitaji sana kulikamata kila wazo baya ,mtazamo mbaya, mwonekano usiofaa na kuvibadilisha kwa vile vitakavyoweza kutuletea maisha kwetu sisi, kwa kusema kutuletea maisha namaanisha; kutuletea furaha, amani, uvumilivu, utu wema, ukarimu uungwana na kujidhibiti binafsi.
25. Kuwa bora kuliko sawa; Pale mtu anapokuuliza unaendeleaje ,sema “vizuri sana”( huku ukiwa na tabasamu na ukimtazama machoni) badala ya kusema “sawa” au vizuri kidogo n.k. Mapema sana, inaweza kuwa ni tabia na kubadilisha mtazamo wako na kuwasaidia wengine pia.
26. Jipe mazungumzo binafsi; Kila siku asubuhi unapojitazama katika kioo; rudia kusema “ nachagua kuwa mtu ninayetaka kuwa na kufanya tofauti katika maisha yangu na maisha ya wengine”.
27. Anza kila siku upya; Unaweza kuboresha maisha yako ya sasa kwa kuachana na mambo yako yote yaliyopita. Muda mwingi unaotumia katika kufikiria kuhusiana na ungekuwa, ungehitaji kuwa, ungeweza kuwa ya mambo yako yaliyopita, ndivyo utakuwa na muda mdogo sana katika kuishi katika wakati uliopo. Hakuna kitu chochote kile unachoweza kukifanya ili kuifuta au kuibadili hali iliyopita. Lakini kwa uhakika unaweza kuyafanya maisha yako ya baadaye kuwa bora na yenye kuvutia, unaweza kuanza sasa.
28. Pangilia kazi zako; Weka maisha yako katika mpangilio. Vitu vya kurudishwa rudishwa au visivyofanyiwa kazi huyafanya maisha yetu kubakia kuwa maisha ya vitu vingi na kuweza kutuzia sisi watu tunaotaka kuwa. Pangilia mambo yako ,Jiwekee vipaumbele katika kazi zako. Chagua kazi moja na maliza kuifanya kwa wakati uliopangwa, na baada ya hapo ndipo utakapoweza kufanya kazi nyingine. Usifanye mambo mengi kwa wakati mmoja kwani mshika mawili moja umponyoka.
29. Kuwa na Shukrani ; Kuwa na shukrani ni jambo la muhimu sana katika maisha yetu ,wengi wetu huwa tunashindwa kufanikisha malengo yetu au yale tunayoyataka kwa sababu tu ya kukosa shukrani. Unapoamka asubuhi toa asante kwa ajiri ya kitu fulani unachokishukuru. Na wakati wa usiku kabla ya kulala toa asante kwa ajiri ya unachoshukuru. Kwa njia hii ,utakuwa unaianza na kuimaliza siku yako kwa shukrani, jambo ambalo ni la muhimu sana katika mafanikio.
30. Vitendo; anzisha nidhamu moja ndogo na kisha ujenge juu yake kila siku. hata kama hautoifanya kwa njia zote .kila wakati unapoifanyisha mazoezi nidhamu hiyo ,ndivyo itakavyojijenga yenyewe na kuweza kufikia hatua kuwa tabia. kwa mfano; unaweza kujiwekea nidhamu ya kujisomea kitabu kimoja kila wiki.
31. Wewe ndiye mwenye mamlaka; hakuna mtu yoyote anayeweza kukufanya ujisikie kuwa duni au wa hali ya chini bila ya ruhusa yako.
32. Kabiliana changamoto kwa ujasiri; Maisha yetu yamejawa na changamoto nyingi sana, lakini namna unavyokabiliana na changamoto hizi ndivyo kunavyofafanua safari yako. Chagua kuwa na furaha, chagua kuwa mwenye matumaini. Chaguzi hizo ndizo zitakufanya kuwa mtu mwenye nguvu na kuweza kupambana na changamoto kwa ujasiri.
33. Samehe ubaya; fanya maisha yako kuwa bora sasa kwako binafsi na kwa wengine kwa kujifunza kusamehe, msamehe kila mtu kwa mambo yaliyopita, na hata yaliyopo waliyokutendea. Samehe kila mtu kwa ubaya wowote waliokutendea .Na kama kuna mtu alikukwaza hapo nyuma msamehe,. kusamehe kunaweza kujenga uhusiano wenye nguvu na wa kudumu katika biashara au mahusiano binafsi. kuwa mtu mkubwa ni udhibitisho wa uongozi wenye nguvu.
34. Lisha ubongo wako; Ili kupata matokeo mazuri katika maisha unahitaji kuingiza taarifa nzuri katika ubongo wako, tunafanya hivyo kwa kuingiza taarifa chanya. Sio taarifa hasi, ikiwa kwa kusikiliza taarifa ya habari kila siku, kusoma magazeti au kwa kusikiliza mazungumzo katika redio, unapata hisia za kwamba nyota inaanguka, hisia za mapigano, mauaji n.k. Subiri! Kadri unavyozidi kujihusisha kwa muda mrefu katika taarifa hasi kama hizi ndivyo utakavyozidi kubakia katika hapo maisha yako, kwenye mambo yaliyo hasi. Na ndicho utakachokijenga katika maisha yako. Kumbuka, ingiza katika ubongo wako taarifa zile zitakazo kusaidia kufanikisha Malengo yako.
35. Pambana na hofu; hofu ni kitu kinachodhoofisha sana katika ulimwengu huu. Hofu inatuzuia sana kuishi maisha tunayotaka kuishi. Mbinu sahihi ya kupambana na hofu ni kwa kufanya tu. Ni muhimu kila mtu afikirie kuhusiana na hili; “ Ni nini ungekuwa unafanya ikiwa ungelijua usingeweza kushindwa? ”fikiria tu nini ungeweza kufanya. Hofu ni adui mkubwa wa mafanikio yetu katika maisha.
36. Tenda kwa kusudi ; kujua kwa nini unafanya hicho unachokifanya. Kutakuwezesha kuongozwa na shauku. Kutakuinua pale utakapoanguka. kutawahamasisha na wengine kuungana nawe.
37. Ondokana na kushindwa; wakati Unapoamua na kuamini kuwa kushindwa ni suala la muda mfupi, litakuwa ni la muda mfupi. Wakati unapoamua na kuamini kuwa kushindwa kutakuharibu, kutakufanya hivyo.
38. Kuna ukweli katika jina; Sema jina la mtu mara kwa mara na katika muito wa kudhibitisha. Hiki kinaonekana kuwa ni kitu kidogo sana kinacholeta tofauti kubwa katika watoto, vijana na hata watu wazima. Kitendo hiki kidogo cha kumthamini mtu kwa kumwita jina lake kunakofuatana na kutia moyo au faraja kutajenga uaminifu na kusababisha watu wastawi.
39. Fanya tu!; kuna njia moja ya kuboresha maisha yako sasa ..ishi maisha yako! usiogope kuruka kwa kutumia ndege, kwa kutia nanga meli, au kwa kuendesha treni. ishi maisha yako kama ikiwa maisha yako yana maana.
40. Weka umakini juu ya kile unachokitaka; fikiri kuhusu unachokitaka, sio usichokitaka. Linda sana mawazo yako kwa uangalifu, kwa sababu mawazo yako yanajenga maisha yako na uzoefu wako.
41. Kuwa mfano wa kuigwa; Kuwa mfano bora wa kuigwa kwa kila mtu ,kuwa mfano bora wa kuigwa kwa watoto wako. Sio tu wataiga kila kitu unachokifanya, lakini pia hata yale usiyoyafanya.
42. Jifunze kwenye imani; Kuwa katika mazingira magumu pamoja na wale uliopata kutambua kuwa ni wenye kuaminika na wapo karibu nawe katika maisha. Hii itakusaidia sana katika kuendeleza uhusiano wa dhati na kuweza kusababisha mazungumzo yenye maana.
43. Chagua kufanya tofauti; Chagua kufanya tofauti katika kila jambo unalolifanya na katika kila sehemu utakayoingia, hakikisha kila kitu unachokifanya unakiacha kuwa bora kuliko ulivyokikuta .Paache mahali pakiwa bora kuliko ulivyopakuta. Chagua kufanya tofauti katika maisha ya kila mtu unayekutana naye, mwache akiwa mwenye shauku kubwa ,matumaini mapya na hamasa kubwa kuliko ulivyomkuta.
44. Kuwa mtu wa watu; Jifunze kutoka kwa kila mtu, zungumza na kila mtu, saidia watu. kwa kufanya hivi utaweza kupata kusudi na kujiamini, na kukusaidia kuendeleza ujuzi mpya pamoja na kufanikisha kila lengo unaloweza kulifikiria wakati unapokuwa unayajaza maisha yako, pamoja na uzoefu mkubwa na matokeo makubwa kuliko kufanya peke yako.

Post a Comment