NI RUKSA KUKATA TAMAA KATIKA MAENEO HAYA MAWILI
Habari
za siku mpenzi msomaji wa mtandao huu wa MTEGACHEM-IT. Ni matumaini
yetu kwamba unaendelea vyema kabisa licha ya changamoto na majukumu
mbalimbali tunayokumbana nayo kila kukicha, pole sana rafiki na
usichoke kupambana. Mara baada ya kusema hayo tugeukie kwenye makala yetu ya
leo. Kama ujuavyo kwamba ni kawaida ya mtandao huu kuwa na utaratibu maalumu wa
kushirikisha wasomaji wake mambo mbalimbali ya kujifunza na kuhamasika. Hilo
ndio lengo kuu la mtandao huu yaani kuwashirikisha ndugu zetu kile tunachojifunza
na kukipitia. Kwani siri ya maisha ni kutoa. Kutoa ndio dhumuni la kila maisha
ya mmoja wetu katika dunia hii. Na sisi kwa kulitambua hilo ndio maana kila
siku tunakuja na kitu kizuri na kipya cha wewe kujifunza. Kwa hiyo, tunapenda
na wewe uungane nasi katika safari hii ya utoaji kwa kutusaidia kuwafikia wengi
zaidi ili waweze kutembelea mtandao huu kwa kuwashirikisha baadhi ya makala
zetu iwe kwenye mitandao au ndani ya jamii yako ili nao waweze kujipatia mambo
haya mazuri unayoyapata. Tutashukuru sana ikiwa utachukua hatua mara moja sasa katika
kuwashirikisha na wenzako. Na kama nilivyokwambia awali kutoa ndio siri ya
maisha na wale wanaotoa iwe misaada, mawazo yao n.k wataongezewa zaidi
kulingana na kile wanachokitoa. Yaani tunavuna kile tunachokipanda. Naona
nisiende mbali zaidi katika kukizungumzia kitu ambacho sio mada yetu kuu ya
leo. Mada yetu ya leo sio kuhusiana na utoaji ila nitakuja kulizungumzia hili
hapo mbeleni.
Katika makala yetu ya leo nakwenda
kuzungumzia kuhusiana na suala la kukubali kushindwa katika kile unachokifanya au upi ni wakati
sahihi wa wewe kuacha kufanya jambo ulilokuwa ukilifanya. Naona mpaka hapo
utakuwa unashangaa kwa nini nazungumzia ukubali kushindwa wakati kwa miaka
kadhaa sasa nimekuwa nikihubiri na kuwahimiza wengi kutokukata tamaa. Ni haki
yako kushangaa ila litakuwa ni jambo la muhimu zaidi ukaendelea kusoma makala
hii mpaka mwisho ili uweze kung’amua ni nini hasa ninachotaka kukueleza na kumaanisha.
Na ni matumaini yangu mara baada ya wewe kumaliza kusoma makala hii utakuwa
umenielewa kwa kiasi fulani na utakuwa umefanikiwa kupata kitu cha kwenda kukifanyia
kazi. Karibu katika mada yetu ya leo..
Kama tujuavyo kwamba siri mojawapo inayochangia
mafanikio ya watu wengi zaidi
duniani ni ile hali ya kutokukata
tamaa, yaani kutokubali kushindwa katika kila jambo wanalolifanya au wapambane
mpaka dakika ya mwisho ili wafanikiwe kupata kile wanachokitaka katika maisha
yao. Nami kwa kulitambua hilo, kwa zaidi ya miaka miwili sasa nimekuwa nikiwasihi
wasomaji wangu na wewe ukiwa mmoja wapo kamwe wasikubali kukata tamaa mpaka
tone la mwisho ili tuweze kuona ndoto zetu zikitimia, yaani tupambane mpaka
mwisho.
Sasa Geofrey, ikiwa umekuwa hukitusii
kutokukata tamaa iweje leo uje na mada ya kukubali kushindwa? Una haki ya
kuniuliza hivyo ili naomba unisikilize kwa makini..
Watu wengi sana katika jamii zetu kwa zaidi ya miongo kadhaa sasa
wamekuwa wakihimizwa kutokukata tamaa au
kutokuacha kufanya jambo mpaka wafanikiwe,
kwa maana nyepesi tunaweza kusema kwamba wameambia wasikubali kushindwa.
hivi unajua sababu ya uwepo wa hali hiyo? Sababu ni kwamba; jamii yetu imekuwa
ikiwachukulia watu wanaokata tamaa kama watu ambao hawatokwenda kufanikisha
jambo lolote lile katika maisha. yaani watu hao hawatoweza kufanikiwa kabisa katika
maisha iwe kwenye jambo dogo au kubwa. ila kwa upande wangu nadhani huu ndio
wakati sahihi wa jamii zetu kuanza kufunguka na kuachana na imani potofu, yaani
imani zisizokuwa na manufaa yoyote kwetu. Kwani wakati mwingine inatubidi
tukubali tu kushindwa hasa wakati tunapokuwa tukitafuta kitu tunachopenda kukifanya (passion), na wakati tunapokuwa kwenye mazingira hasi. Na kuna nukuu maarufu
imekuwa ikitumiwa sana na wengi japokuwa wengi wanaoitumia wamekuwa wakiipuuza
ila ina maana kubwa sana ndani yake. Nukuu hiyo si nyingine bali ni kwamba”
asiyekubali kushindwa si mshindani”. Hiyo ni nukuu nzuri na yenye maana kubwa
ndani yake ikiwa utaielewa kwa upana zaidi.
Wakati
sahihi wa kukata tamaa.
Hapo kabla nimekwambia kwamba wakati sahihi
wa wewe kukata tamaa ni wakati unapokuwa unatafuta kile unachopenda kukifanya
(passion) na wakati unapokuwa kwenye mazingira hasi. Na yafuatayo ni maelezo
machache ya kwa nini ni ruksa kukata tamaa kwenye maeneo hayo mawili.
1.Unapokuwa
unatafuta kile unachopenda kukifanya; kwa kweli ni ruksa tu kwako kukata tamaa
wakati unapokuwa unatafuta kile unachopenda kukifanya. Sasa swali muhimu
linalokuja hapa ni je wakati upi ukubali kukata tamaa? Ni pale unapokuwa
haufanyi kitu unachokipenda au ukuwahi kukipenda kukifanya hapo kabla. kufanya
kitu usichokipenda ni sawa na kupoteza muda wako bure, na ikiwa hauna furaha
katika kile unachokifanya basi hakuna hitaji la kuendelea kufanya kitu hicho na
ni muhimu ukaachana nacho kwani hautokuja kufanikiwa. Na kama utawaangalia kwa
makini watu wote wenye mafanikio katika maisha utakuja kugundua kwamba watu hao
wamefanikiwa kutokana na kufanya kile wanachokipenda na si vinginevyo. Kwa hiyo
kuanzia sasa ni ruksa kukata tamaa unapofanya jambo usilolipenda.

Post a Comment