Header Ads

Kama unashindwa kuamua ni biashara gani ufanye, soma hapa !!


Watu wengi wakiulizwa ni biashara gani inaweza kukupatia fedha kwa urahisi, hujibu kwa kuangalia watu waliofanikiwa kupitia biashara mbalimbali na kuzitaja biashara hizo kama ndiyo zina faida kubwa. Tambua kwamba biashara yeyote inaweza kufanikiwa ikiwa itapata wateja wengi wakutosha. Hivyo suala la msingi, sio biashara gani ya muhimu, bali ni vigezo gani vya msingi. kabla hujaacha kazi zingatia yafuatayo:

Tafuta mshauri (mentor)
Pata mshauri (Mentor) atakayekusaidia katika safari ya Ujasiriamali. Mshauri ni mtu ambaye amefanikiwa kwenye jambo fulani na ana uwezo wa kuwasaidia/kuwaelekeza watu wengine wafanikiwe kama yeye.

Fanya kazi kwa mtu aliyefanikiwa
Fanya kazi kwenye biashara ya mtu aliyefanikiwa na ambaye unataka kuja kuwa kama yeye. Wakati mwingine, njia ya mkato ya kujifunza biashara ni kukubali kutumika chini ya mtu mwingine ili ujionee moja kwa moja uendeshaji wa biashara kabla hujaamua kuingia moja kwa moja

Chunguza siri za biashara zinazofanikiwa
Jaribu kuchunguza siri za biashara zinazofanikiwa na mifumo iliyopo nyuma yake Watu wengi huwa na wazo la bidhaa ya kuuza au hata kutengeneza lakini mara nyingi huwa hawana ujuzi wa kutengeneza mfumo mzuri wa uletaji wa faida.

 Jenga tabia ya kuuliza  maswali ya msingi kwa wajasiriamali waliofanikiwa.
unapopata nafasi ya kuwa na mtu aliyefanikiwa, jipe moyo mara kwa mara halafu uliza swali hili: “Je siri ya mafanikio yako ni nini?” Utashangaa jinsi ambavyo watu wengi si wachoyo wa siri zao za mafanikio ili mradi tu uulize katika mazingira mazuri yenye heshima na hekima.

Jijengee uwezo wa kuuza  (everyone is a sales person -brian tracy)
Jenga Uwezo wa kuwashawishi watu waweze kununua bidhaa yako au kutumia huduma yako ndiyo uweze kusimama katika Ujasiriamali

No comments

Contact us:Email:godfreymtega@gmail.com/WhatsApp-+255758297744/+255716824009 . Powered by Blogger.