Header Ads

Umuhimu Wa Kutafuta Ukweli Wa Kila Taarifa Uipatayo.

Habari za wakati huu ndugu msomaji wa mtandao huu, ni matumaini yangu kuwa hu mzima na unaendelea vizuri katika kuhakikisha kuwa unapambana ili kujiletea mafanikio. karibu tena Leo tujifunze kwa pamoja kuhusiana na umuhimu wa kutafuta ukweli wa taarifa tunazopewa au kuzisoma sehemu fulani.

Leo hii kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia kumekuwa na namna mbalimbali za upashanaji habari kama vile kupata habari kupitia redio,TV, blog,magazeti na vyombo vingine vya habari. Sisemi kuwa vyombo hivi havifai lakini nachotaka kusisitiza hapa ni umuhimu wa kutafuta ukweli wa taarifa ili kujiridhisha na kufanya maamuzi yenye manufaa kwetu.mfano  kama utakuwa mfuatiliaji mzuri wa taarifa mwezi uliopita kuna taarifa zilizagaa kuwa mgombea uraisi wa marekani bwana Donald Trump kwamba kauwawa kwa kupigwa risasi, lakini taarifa hii ilikuwa ya uongo. Kutokana na watu kutokuzingatia umuhimu wa kupata ukweli wa taarifa basi wakaanza kusambaziana na vitu kama hivyo.


Katika maisha ya kawaida haya tunayoishi huku tukiwa ni watu wenye kutaka mafanikio ni muhimu basi tukazingatia katika kutafuta ukweli wa taarifa.Kuna taarifa katika uwekezaji, kilimo,biashara hata malezi na mahusiano zimekuwa zikitolewa huku zikiwa zimejaa upakwaji rangi mkubwa sana hivyo kama hauko makini kutafuta ukweli wa taarifa hizo basi unaweza kujikuta umefanya maamuzi ya kuingia katika biashara,kilimo au hata ufugaji kichwa kichwa na matokeo yake ukaja kuambulia patupu.

Unachotakiwa leo hii usiwe mtu wa kukurupuka bali uwe ni mtu wenye kutulia na kufanya maamuzi ya maana ambayo yatakuletea tija na mafanikio ya kudumu katika maisha, leo hii watu wengi tumekuwa wenye kujichanganya kisa tu kutokufanyia uchunguzi taarifa unayopewa, leo hii kuna mtu akipewa taarifa juu ya kilimo labda cha nyanya kuwa kinaripa basi atakimbilia huko Mara moja,mtu huyu huyu akija kusikia kuwa kilimo cha pilipili hoho kabla hata hajamalizana na nyanya atakimbilia huku pia, akija kupewa taarifa kuhusu biashara ya mbao pia atataka.Sasa huku ndio kutokuwa makini na taarifa na lazima uelewe kuwa sio kila taarifa inakuhusu wewe, bali zingine zako na zingine za wengine.

Umuhimu wa kufanyia uchunguzi taarifa uliyopewa ni kuwa unapata taarifa za msingi juu ya kile kitu unachokuwa umearifiwa, leo hii kama nilivyokuambia hapo juu kuwa taarifa nyingi zimejaa upakwaji rangi ni kutokana na kuwa taarifa hizi zimekuwa ni za upande mmoja yaani zinakuwa zina upande wa faida tu bila upande wa hasara, sasa ukiwa sio mtu wa kutafuta ukweli wa taarifa utajikuta na wewe umejiingiza kichwa kichwa bila kuzingatia wala kujiandaa kwa hasara matokeo yake ni kuwa unakuja kufulia na kupata anguko kubwa la kimaisha na hapa hakuna mchawi bali mchawi ni wewe mwenyewe kwani hukutaka kutafuta ukweli wa  taarifa.

Hivyo basi kwa kila taarifa unayoipata hakikisha kuwa unaifanyia uchunguzi wa kina na kujiridhisha ndipo uamue nini cha kufanya juu ya taarifa husika. Usiwe mtu wa kuendeshwa na taarifa bali wewe kuwa mtu mwenye uwezo wa kupembua taarifa husika na kuweza kuamua ufanye nini. Jambo jingine la kuwa makini nalo ni juu ya blogs za udaku ambazo kwa sasa hapa Tanzania zinafanya vizuri, ikiwa wewe ni mtu unayetaka mafanikio zisikupotezee muda hata siku

No comments

Contact us:Email:godfreymtega@gmail.com/WhatsApp-+255758297744/+255716824009 . Powered by Blogger.