Header Ads

VIDEO: Uchambuzi wa Edo Kumwembe kuhusu dau la Pogba Man United na changamoto atakayokutana nayo

Baada ya kusajiliwa kwa dau la usajili wa rekodi ya dunia la Pound milioni 100 akitokea Juventus ya Italia kurejea Old Trafford Paul Pogba kesho August 19 atakuwa na mtihani wa kucheza mechi yake ya kwanza na Man United baada ya kumaliza adhabu yake ya kukosa mechi moja ufunguzi wa EPL dhidi ya AFC Bournemouth.
Katika mchezo wa kesho anaotarajia Paul Pogba kucheza dhidi ya Southampton katika uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford, wengi wanasubiri kuona atafanya nini kiungo huyo hususani baada ya kuvunja rekodi ya dunia ya usajili, Ayo TV imempata mchambuzi wa Edo Kumwembe ambaye anaelezea dau la Pogba na changamoto atakazokutana nazo katika maisha yake ya soka kwa kuuzwa kwa dau hilo.
“Kuhusu dau la Pogba hakuna uhalisia wowote wa uwezo wake na dau hilo, kwa mimi naona Pogba ni mchezaji ambaye ningemnunua kwa pound milioni 50 ila sio 100, kwanza kumnunua Pogba kwa pound milioni 100 humtendei haki kwani utampa wakati mgumu sana wa yeye kutaka kudhihirisha kuwa anastahili kununuliwa kwa dau hilo”


No comments

Contact us:Email:godfreymtega@gmail.com/WhatsApp-+255758297744/+255716824009 . Powered by Blogger.