Habari 5 ‘HOT’ kwenye TV za Tanzania August 18 2016
Habari zilizopewa airtime kwenye TV za Tanzania unazipata hapa mtu wangu Kama ulikosa time ya kuangalia taarifa ya Habari ya August 18 2016 usijali Millardayo.com inakupa fursa ya kuziangalia Habari tano ‘Hot‘ kupitia TV za Tanzania.
Habari kutoka ITV
Wakadiriaji majenzi watakiwa kuepuka rushwa na kulinda taaluma yao.
Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano (Mhe.Prof.Makame Mbarawa) amewaeleza wakadiriaji hao kuwa na mkadiriaji yeyote atakae kosa uwadilifu serikali itamfutia usajili na kuongeza kuwa ni bora kuwa na wataalamu wachache watakaofanya kazi na walio waadilifu pia kuwa na viwango vya kimataifa.
Habari kutoka Azam TV
Udhibiti dhidi ya matumizi ya Tumbako bado.
Waziri wa afya (Mhe.Ummy Mwalimu) amesema haya kuhusu utumiaji wa Tumbaku unaoendelea nchini akiongelea mkakati wa serikali kupunguza matumizi ya Tumbaku kufikia asilimia 25 mpaka mwaka 2030
>>>’ Tukiongeza kodi za bidhaa za Tumbaku kwa asilimia 10 kwa miaka mitano, kwanza tutaongeza mapato ya serikali kwa asilimia 39.9 mpaka 47.5 lakini pia tutaokoa vifo vya watanzania takriban elfu 63 kwahiyo kodi ndiyo moja wapo ya njia bora na sahihi za kudhibiti matumizi ya Tumbaku nchini‘- Waziri wa afya (Mhe.Ummy Mwalimu)
Habari kutoka Star TV
Mgogoro wa Ardhi
>>>‘Haiwezi kuwa na haitatokea chini ya awamu ya tano kwamba mtu mgeni atapita kila mahali kwenye kona ya nchi hii atakusanyakusanya ardhi alafu atachukua hati , nchi hii haiwezi toa hati kwa namna hiyo‘- Waziri William Lukuvi
Habari kutoka Azam TV
Rais Magufuli amekutana na katibu Mkuu wa EAC Ikulu Dar es salaam
>>>’Nimemweleze Rais kwamba tuna project nyingi sana na inahusiana vizuri na vipaumbele vyetu,na tenatunangalia jinsi tunaweza kufanya kazi na wananchi wa Eact Africa wapate faida‘- Katibu Mkuu wa EAC ( Liberat Mfumukeko)
Habari kutoka TBC
Amani Tanzania, viongozi wakubwa wa dini nchini wameongelea juu ya swala hili
>>>’Ni vizuri basi watanzania hii tarehe moja tuwe na tahadhari nayo endapo serikali itajipanga kupokea maandamano hayo na kuyaruhusu watanzania waandamane, lakini kama serikali itabaki na msimamo wake kuwaingiza watanzania barabarani wakaja kupata ulemavu na kuumia na pengine vifo vikatokea si jambo la busara‘ – Mwenyekiti kamati ya Amani Dar es salaam (Sheikh Alhad Musa Salum)
Post a Comment