Dodoma yatajwa kuwa kinara wa viashiria vya ugonjwa huu
Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya habari kubwa iliyoandikwa kwenye magazeti ya August 17 2016 ni hii kutoka gazeti la MTANZANIA yenye kichwa cha habari ‘Dodoma yatajwa kinara viashiria’
#MTANZANIA Dodoma imetajwa kuwa na viashiria vya juu ktk maambukizi ya UKIMWI ikilinganishwa na mikoa mingine
Mkoa wa Dodoma umetajwa kuwa na viashiria vya juu katika maambukizi ya UKIMWI ikilinganishwa na mikoa mingine. Hali hiyo imetokana na kuwepo kwa vitu kadhaa vinavyowakutanisha vijana vikiwamo vyuo na sehemu za starehe.
Akizungumza na Gazeti la Mtzanzania, mratibu wa programu za kanda za Afrika,Renatus Kihongo alisema utafiti uliofanywa mwaka 2012 unaonesha vijana wengi katika manispaa ya Dodoma wanatumia muda mwingi kwenye starehe jambo ambalo ni linatishia uwepo wa maambukizi ya ugonjwa huo.
Utafiti huo ulifanywa na Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania ‘TACAIDS’ viashiria vya maambukizi ya UKIMWI vipo juu kwa vijana kati ya miaka 15 hadi 24 ambapo wanafunzi wa vyuo vikuu ndio wanaonekana kuwepo katika viashiria hivyo.
Kihongo alisema mkoa wa Dodoma kitaifa upo katika nafasi ya 22 kwa kuwa na maambukizi ya UKIMWI……..>>>’Mara nyingi sehemu yoyote sehemu yoyote yenye maendeleo inakwenda sambamba na viashiria vya maambukizi ya UKIMWI kutokana na kuwepo na muingiliano mkubwa wa watu ambao baadaye hujenga uhusiano’
Source: MTANZANIA
Unaweza kupitia habari nyingine kwenye magazeti ya Tanzania leo August 18 2016
#MWANANCHI Lubuva asisitiza kuwa kikatiba NEC ni huru na hajawahi kupewa maelekezo na Rais wakati wa uchaguzi mkuu
#MWANANCHI Lissu ambaye ni wakili wa Bulaya, apangua maombi ya wananchi wanne wanaopinga matokeo ya ubunge wa Bulaya
#MWANANCHI Tanzania imekuwa nchi ya kwanza bora duniani kati ya 10 zitakazotembelewa na watalii mwaka huu
#MWANANCHI KCMC yalalama kuwalipia wagonjwa, mwaka jana pekee imetumia mil 306 wagonjwa wenye msamaha wa matibabu
#MWANANCHI Serikali kuzuia uingizaji wa saruji kutoka nje baada ya uzalishaji wa ndani kutosheleza mahitaji
#HabariLEO Kaimu mkurugenzi TanzaniteOne avuliwa madaraka kwa tuhuma za kuwanyanyasa wafanyakazi wa kampuni hiyo
#HabariLEO Kiwanda cha kutengeneza vifaa vya zimamoto chazinduliwa kitasaidia kutunza mamilioni ya kuagiza vifaa nje
#MTANZANIA Taasisi ya tiba ya moyo ya Jakaya Kikwete inakabiliwa na upungufu wa madaktari kwa kiwango cha 50%
#MTANZANIA Zaidi ya mil 190 za ulipaji fidia Mbarali, Mbeya zinadaiwa kutafunwa na watendaji wa halmashauri hiyo
Post a Comment