Header Ads

JINSI YA KUTOA iCloud LOCK KWENYE iPhone 6 5s 5c 5 4s 4 MOJA KWA MOJA



Kuna mdau amenifanya niandike hiki nachoenda kuandika kwa sasa, Ahsante sana kwa kunifanya nipate jambo la kushare na wadau wangu kupitia huu ukurasa wangu.
  Leo nataka nikupe tu njia rahisi ya  kutoa iCloud lock kwenye simu za  iPhone 6 5s 5c 5 4s 4. kumbuka kuwa unapokumbana na tatizo la icloud lock ni dhahiri kuwa unakuwa huna uwezo wa kutumia kiaa chako, na hii inatokea pale ambapo unakuwa umesahau password zako au pale napo kuwa umenunua simu used kupitia kwa mtu au hata kwenye mitandao, ipo mitandao mingi sana inayouza vitu online ila nisingependa kuitaja hapa..
kuna njia mbili za kuweza kutoa icloud lock kwenye simu hizi

NJIA YA KWANZA
 Ni kwenda kwenye store yoyote ya Apple iliyo karibu na wewe huku ukiwa  na ushahidi wa kutosha kutoka kw mmiliki wa simu ambaye amekuuzia. mfano kama mliandikishiana au kama ulinunua mtandaoni basi ni vyema ukaenda na risiti ili kuthibitisha umiliki wa hiyo simu kutoka kwa aliye kuuzia. hii ni njia rahisi sana kwani kinachotakiwa ni uthibitisho tu. tatizo kubwa linalo jitokeza katika njia hii ni kwamba wengi wetu hupenda kununua simu za mikononi na pia si watunzaji wa risiti

NJIA YA PILI
Kama njia hiyo hapo juu imeshindikana basi njia nyingine ya kutoa hizo lock ni kufanya kitu kinachotwa  Bypass iCloud Account activation Lock  and Disable iCloud Lock screen 
  hivyo basi ili kufanya njia hii fata maelezo haya
angalia aina ya simu unayo tumia mfano iphone 4s
 baada ya hapo nenda sehemu ya kupigia simu kisha piga *#06# utaletewa imei number za simu yako kisha zicopy pembeni
 baada ya hapo nenda kwenye website ifuatayo  Official iCloud Activation Lock Removal
jaza  taarifa zako kama ifuatavyo
Handset type: chagua saina ya simu  unayotumia  mfano iphone 4s
IMEI/Serial: hapo jaza imei za simu yako ambazo ulikuwa umezicopy pembeni
kisha bonyeza add to cart kisha itafunguka page itakutaka uhakikishe na kuingiza email yako
 huduma hii ni ya kulipia na inagharimu  £ 19.99 na inachukua siku 1 hadi tatu

baada ya muda utapokea email itakayo kujulisha  kuwa Activation Lock zimeondolewa kwenye simu yako
baada ya hapo utahitajika kutengeneza account ya kwako ya icloud ya find my phone huku ile ya mara ya kwanza itakuwa imeondolewa kabisa
 njia hii inaweza kutumika kwenye iphone zote pamoja na ipad pia. kumbuka njia hii sio ya bure ni njia ambayo inatumia gharama.

No comments

Contact us:Email:godfreymtega@gmail.com/WhatsApp-+255758297744/+255716824009 . Powered by Blogger.