Header Ads

Jifunze kutengeneza bidhaa za viwandani kwa vitendo.

Karibu mpenzi mfuatiliaji wa blog yako pendwa Mtega Blog.Leo nakuletea somo zuri la utengenezaji wa sabuni ya maji.Hii inaweza kukuinua kiuchumi.Karibu katika somo letu
Utengenezaji wa sabuni ya Maji
Matumizi ya sabuni hii.kufua,kudekia.Ukitaka kuoshea vyombo usiweke Formalin
A:Malighafi
1.Sulphonic acid
2.Sless
3.Soda ash
4.Glycerine
5.Manukato/Perfume
6.Rangi a sabuni
7.Maji
8.Chumvi ya kiwandani
Mambo muhimu ya kuzingatia:Vaa gloves,vaa nguo ndefu.

Jinsi ya Kutengeneza
1.Weka sulphonic acid lita moja kwenye chombo chako cha plastic.
2.Weka Sless nusu lita
3.Weka soda Ash vijiko vinne vya chakula,anza kukoroka kuelekea upande mmoja.
4.Weka maji Lita 20 endelea kukoroga
5.Weka glycerine vijiko 3 vya chakula.
6.Weka formalin vijiko 2 chakula kwaajili ya kutunza sabuni yako.
7.Weka perfume/manukato vijiko 2 chakula
8.Weka rangi kutokana na mahitaji ya wateja wako.
9.Weka chumvi ya kiwandani nusu kilo(Weka kidogo kidogo huku unakoroga).Sabuni yako itaanza kua nzito.
Mpaka hapo sabuni yako tayari kwa matumizi/Packaging kwa ajili ya kuuza.

Endelea kufuatilia Makala zetu.
Mwandishi/Mkufunzi
Godfrey Mtega(Mkemia)
0758-297744/0716-824009
Facebook:Godfrey Mtega
Instagram:mtegablog
Youtube:MTEGA TV
Location:Dodoma

Usisite kuwasiliana nasi popote ulipo kwaajili ya kujifunza bidhaa zifuatazo kwa vitendo.(Tunafundisha vikundi vya wajasiriamali,Vyuoni,Mashuleni n.k)

  • Sabuni za miche
  • Sabuni za magadi
  • Sabuni za kunawia mikono
  • Sabuni za kuogea
  • Tiles cleaner
  • Shampoo
  • Mafuta ya kuapaka
  • Sabuni ya unga
  • Dawa ya choo
  • Mishumaa n.k

No comments

Contact us:Email:godfreymtega@gmail.com/WhatsApp-+255758297744/+255716824009 . Powered by Blogger.