Header Ads

Geuza Smartphone Yako Kuwa Computer

Unajua Kama Ukiwa Na Smartphone Unaweza Kuigeuza Ikawa Computer?
Leo Nimekuja na kitu kizuri!
Ni moja ya mambo ya Ukuaji wa teknolojia, hivyo basi sio mbaya baada ya kukushirikisha ukamshirikisha na mwenzako pia;
  1. Ulishawahi kuhisi kuichoka simu au tablet yako kutokana na udogo wake kwenye kuhifadhi mambo yako? (low storage space)
  2. Muda mwingine inakusumbua na kukwambia memory is full huwezi kuweka kitu chochote
  3. Simu yako imejaa vitu vyako vya muhimu sana na hauna Computer na hautaki kuvifuta na pengine hauna sehemu ya kuvitunza
  4. Ukisoma maelezo vizuri utagundua vingi na utapata njia ya kutatua matatizo mengine mengi pengine hata yakazidi hayo niliyoyataja hapo

Ok, sasa basi ninakupa hii kitu hapa, Kuna Cable Mpya kabisa zimetoka juzi juzi zinaitwa “OTG Cables“, kirefu cha OTG ni (On The Go) Kwa hiyo kwa kirefu zinaitwaOn The Go CablesHizi Cable kuna watu hawazifahamu kabisa na hawajui utamu wake. Leo nakudadavulia mambo makubwa utakayoweza kuyafanya endapo una OTG Cable, itazame hapa;

51MX0dwuMZL._SX355_
 
Cable hizi zina pande mbili,
Upande wa kwanza una kichomekeo kama Cha zile chaji za smartphones zetu tulizozizoea, na huu ndio upande unaoingia kwenye simu au tablet na unachomeka kama vile unavyochomeka chaji.

Na upande wa pili wa OTG Cable kuna tundu kubwa la kuchomekea vitu vya asili za USB kama vile flash, lakini kwa upana zaidi naomba nieleze maana kuu ya hili tundu (kwa kitaalamu huwa tunaliita USB Female Port), na linaruhusu kuchomekwa vifaa mbalimbali kwa matumizi tofauti tofauti ila tu vifaa hivyo viwe vya aina ya USB, mfano kama FlashiKeyboardExternal Hard Disk, Speakers n.k.

Sasa basi ukichomeka Cable hiyo kwenye simu au tablet yako kama vile unavyochomeka chaji kwa upande wa kwanza na upande ule wa pili ukachomeka flash, basi utaweza kuisoma kwa ndani ya simu kama vile huwa unasoma memory card yako, tazama picha hapa chini kuelewa zaidi;

CM001_gadgetstuff-data-OTG_STD_2_1024x1024-500x500Unaweza pia kuchomeka External Hard Disk na ukaitumia kwenye simu au tablet yako, kufanya shughuli mbalimbali kama vile kucheki movies n.k, sijamaliza bado;
Kama simu au tablet yako imejaa vitu unaweza kuvihamishia kwenye flash ukavitunza, kwa mfano hauna Computer, unaweza kununua OTG Cable na flash yako ya 16 GB ukaweka vitu vyako kama Picha, Videos n.k na simu yako ikabaki free na ikawa na spidi ile ile kama ya siku ile ulipoinunua, na hapa hautalalamika tena kuwa simu yako ina uwezo mdogo wa kutunza vitu, sijamaliza bado;

Kwa wale tunaotamani sana kuwa na Computer lakini hatuna uwezo wa kuzinunua, lakini tunamiliki Smart Phones Zetu nzuri tu, basi hapa nakupa maujanja, nenda dukani ulizia OTG Cable (Sijui ni duka gani maana simtangazii mtu biashara ila mimi binafsi nilinunua elfu 5 tu ila kuna sehemu ukienda utapigwa mpaka elfu 40, tembelea duka lolote la simu ulizia), ukishanunua OTG Cable, nunua flash zako za 16 GB kama 3 au 5 kama una uwezo, kisha nenda kakopi vitu unavyohitaji kwa mtu mwenye Computer na uviweke kwenye flash yako (mfano flash ya Movies pekeyake, ya madocuments pekeyake, ya miziki pekeyake na ya picha pekeyake, najua ugonjwa wetu vijana na wazee kwa mbaliii ni Miziki, Movies, Kujirekodi Na kupiga Picha hasa kwenye event za kifamilia na hivi vitu hujaza sana simu zetu, hivyo ukiwa na flash zako kama nivyoeleza basi utakuwa salama zaidi, ukiweza hayo basi Ukiwa na simu yako, flash zako, na hiyo OTG Cable ni sawa na kumiliki Laptop, sijamaliza bado;

Utaepuka maswala ya kuhamisha vitu kwa kuchomeka USB cable, au kutumia bluetooth kuhamishiana vitu vyenye saizi kubwa na vingi toka kwenye simu au tablet ya  mtu mwingine bali litakuwa ni swala zima la kuchomeka OTG Cable na flash yako kisha unahamisha vitu kwa kukopy na kupaste, na zina spidi nzuri balaa,sijamaliza bado;

Wale wenye simu kubwa unaweza kuikamilisha simu yako kuwa Computer kwa kuifanya hiyo OTG Cable iweze kuzalisha USB ports nyingine nyingi ili uweze kuchomeka vifaa vingi kwa wakati mmoja kama Speakerkeyboardmouse,external hdd n.k, angalia picha hapa chini;

usb-otg-tricks-things-android-mobile

No comments

Contact us:Email:godfreymtega@gmail.com/WhatsApp-+255758297744/+255716824009 . Powered by Blogger.