Mapishi ya Supu ya makongoro.
Mahitaji
Makongoro (miguu ya ng'ombe) kiasi
Limao 1 kubwa
Kitunguu swaum
Tangawizi
Chumvi
Pilipili
Matayarisho
Safisha
makongoro kisha yatie kwenye pressure cooker. Kisha tia kitunguu swaum,
tangawizi, chumvi,limao na maji kiasi. Baada ya hapo yachemshe mpake
yaive na yawe malaini na pia ubakize supu kiasi inaweza kuchukua kama dk
45 au saa 1 hivi. Baada ya hapo yaipue na upakue supu yako kwenye
bakuli katia pilipili kiasi kisha itakuwa tayari kwa kuliwa.
Note:
Ukiwa unanunua makongoro hakikisha unachukuwa yale yasiyokuwa na manyoya na pia
hakikisha usiyachemshe kupitiliza kwani yakiwa malaini sana utashindwa kuyaenjoy.
Post a Comment