Mapishi ya Maini ya kuku,
Mahitaji
Maini ya kuku 1/2 kilo
Vitunguu vikubwa 2
Hoho 1
Pilipil 1
Limao 1/2
Swaum/tangawizi 1 kijiko cha chai
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Mafuta ya kupikia
Matayarisho
Safisha
maini weka pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu,swaum na tangawizi
pamoja (hakikisha vitunguu visiwe vya brown), kisha tia maini, curry
powder, pilipili, chumvi ,hoho na limao kisha changanya vizuri na
ufunike. Pika mpaka maini yaive na hakikisha yanakuwa na rojo kidogo.
Baada ya hapo ipua na yatakuwa tayari kwa kuliwa na chochote upendacho
kama vile chapati, chips, ugali, wali.
Post a Comment