Mafanikio Na Utajiri Unaotafuta, Yanategemea Sana Kitu Hiki.
Habari
mpenzi msomaji wa MTEGACHEM-IT Ni matarajio yetu ya kwamba umeianza siku hii
ya leo vizuri na upo hapa tayari kwa ajili ya kujifunza mambo muhimu ya kuweza
kubadilisha maisha yako na kuwa mtu wa tofauti.
Leo
hii katika makala yetu ningependa nianze kutoa ushauri hasa kwa wale wanaolalamika
sana kila siku na kila wakati kwamba maisha ni magumu. Najua watu hawa unawajua
vizuri na wamekuwa ni watu wa kulalalamika sana karibu kila siku.
Kama
na wewe ni mmoja wa watu hawa ningependa kukwambia ili utoke hapo unatakiwa
kufanya jambo moja tu, ambalo ni kufanya
kazi kwa bidii zote kana kwamba hutakufa. Fanya kazi na weka juhudi zako zote
hapo. Kwa kufanya hivi itakuwa kwako njia bora kabisa ya kukufanikisha.
Kama
unatembeza bidhaa zako, usijihurumie mwenyewe, pita kila mahali, nenda kila
ofisi uwezavyo kuingia, fanya kama kichaa asivyojihurumia. Usinielewe vibaya.
Wakati unafanya yote hayo kumbuka kutunza afya yako pia. Hiyo kwani ndiyo
itakayokusaidia kuyafikia mafanikio yako.
| WEKA JUHUDI, PESA UTAZIPATA TU. |
Ninachotaka
kusema hapa ni kwamba fanya kazi kwa juhudi zote. Acha kutafuta visingio
vitakavyokuletea uvivu. Jitume huku ukijua kabisa kwamba kazi ndio mkombozi wa
maisha yako yote. Bila kufanya hivyo huna maisha ya kusonga mbele.
Haijalishi
una malengo mazuri kiasi gani, haijalishi wewe ni mbunifu kiasi gani,
haijalishi wewe una vipawa kiasi gani lakini kama tu haujitumi na unategemea
muujiza wa kufanikiwa hilo halitaweza kutokea kamwe kwenye maisha yako hata
siku moja.
Kanuni
hii ni muhimu sana kuitambua. Hakuna ambaye ameifanyia kazi kiukamilifu
ikamuangusha. Kwa wote wenye bidii ukiongeza na ubunifu mafanikio makubwa huwa
yapo upande wao. Kwa anayetumia kanuni hii, hakuna mashaka ya kutajirika. Hakuna
mashaka ya kuwa maskini tena.
Waangalie
wale watu wote walioweka bidii na juhudi katika mambo yao nyakati zote nini
kiliwatokea? Bila shaka ni mafanikio makubwa. Huo ndio ukweli ambao hauwezi kupingwa.
Unaweza ukaangalia historia au vitabu vya kuhamasisha vyote vimeongelea jambo
hilohilo.
Hivyo,
utaona wale wote wenye bidii huwa ni watu wasiochoka , wasiotulia, wala kuwa na
utulivu mkubwa nafsini mwao mpaka wamepata kile walichokuwa wakikihitaji katika
maisha yao. Kitu gani kinakuwa kimewasaidia ni bidii yao.
Ili na
wewe uweze kufanikiwa kwa kila jambo, hii ni kanuni mojawapo bora ya mafanikio
ambayo hutakiwi kuitupa nyakati zote. Hakikisha huridhiki wala hutulii mpaka
ufanikiwe unalolitafuta. Fanya kana kwamba ni nafasi pekee ya kulifanya hilo
unalolifanya na haitatokea tena.
Natamani
uwe na kiu kubwa sana ya mafanikio ii ikusaidie kuwa na bidii ya ajabu sana
katika utendaji wako. Ukishaweka ubunifu katika unalolitenda, weka bidii zote
mpaka uone limefanikiwa na hakika litafanikiwa hakuna wa kuweza kulizuia hilo.
Hivi
ndivyo kanuni hii inavyofanya kazi na ni kama vile injini ya kanuni zingine. Bila
kanuni hii zingine zote zaweza kushindwa. Unaweza ukawa una kipaji, mbunifu na
una malengo mazuri, yote haya yanaweza kuwa bure usipoweka juhudi. Kumbuka,
mafanikio yako na utajiri wako unategemea sana bidii yako katika utendaji wako.
Post a Comment