Kama Unataka mabadiliko Makubwa, Anza Kubadili Kitu Hiki Kwanza.
Hii sio
siri sasa, bali ni ukweli ulio wazi kuwa kila mtu anapenda mabadiliko makubwa
katika maisha yake. Ndiyo maana hata moyoni mwako ukijichunguza wewe mwenyewe,
utagundua unapenda mabadiliko na
mafanikio, lakini bado unajiuliza hivi nitapata wapi mabadiliko kwenye maisha
yangu?
Mmh!
Usivyo hata na upendo wa maisha yako mwenyewe ati unajidanganya ‘oh! Mimi siwezi, sio kipaji changu’ na
unabaki kutoa sababu kuwa wazazi ndio chanzo, umekata tamaa na zaidi ya yote
bila hata wasiwasi kila siku unabaki kusema ‘Maisha ni magumu’.
Ni kweli
maisha yanaweza yakawa magumu kama unavyosema sikukatalii, lakini kitu
unachotakiwa ujiulize nani aliyekuahidi maisha ni rahisi? Nani aliyekwambia ati
ukipata kazi nzuri ndio basi kila kitu kimeisha? Au ni nani aliyekwambia
ukipata pesa ndiyo unaweza kufanya mabadiliko yoyote unayotaka?
Haya
ngoja nikuulize wewe mwenyewe kwanza. Ni wangapi wanapesa na hawana hata punje
ya mabadiliko makubwa zaidi wanaishi maisha yaleyale, nyumba ni ileile,
matatizo ni yaleyale. Ni wangapi wanapokea mishahara mizuri lakini baada ya
muda mfupi hata hawajui pesa zilipoelekea.
![]() |
| MABADILIKO MAKUBWA YA MAISHA, YANAANZA NA WEWE. |
Matatizo
yakujitakia mwenyewe usisingizie wengine eti umefanyiwa changa la macho, usianze
kumsema mtu eti amekuloga. Je, ulimwona akikuloga, unachoamini eti huna nyota
na hata sasa bado unabaki kujilinganisha na wengine wala huna msimamo.
Acha
kutingisha kichwa na kuangalia chini kujuta na kujihisi, wewe elewa na tambua
nakueleza mabadiliko sahihi yanapotakiwa kuanzia na ufanye nini ili kuweza
kuyapata mafanikio hayo siku zote za maisha yako na uache visingizio vyako . Ndiyo
unaweza kupata mafanikio makubwa ukitaka.
Hauhitaji
akili za ziada au kutumia nguvu nyingi sana, sababu mabadiliko hayaji tu ‘automatic’, bali mabadiliko yoyote
yanaanza kiakili halafu kimwili. Kama haujajua, huu ndiyo ukweli halisi unataka
mabadiliko ni lazima uanze na wewe mwenyewe kwa kuhakikisha unatoa thamani
inayoendana na mabadiliko unayoyataka.
Ni sahihi
kabisa ninaposema mabadiliko ni lazima yaanze na wewe mwenyewe, kama unabisha
nyosha mkono juu. Huu ni ukweli usiopingika mabadiliko ni kwako mwenyewe
kwanza. Ni lazima ubadilike na kutoa thamani itakayokupa mafanikio unayoyataka,
bila kufanya hivyo sahau kwanza mafanikio.
Kuwa
na viongozi wazuri pekee hawatoshi, kuwa na pesa ndio kabisa sio chanzo pekee
cha kukufanikisha na kukupa mafanikio ya kudumu, usidanganyike. Siku zote
mabadiliko yanaanza na wewe mwenyewe, halafu
ndiyo utaweza kubadilisha historia ya maisha yako na kuacha wengine wakishangaa
kwa sababu walifikiria hautaweza kuja kufanikiwa.
Anza
sasa, kabla ya kuangaza angaza macho sehemu nyingine. Anza kujiangalia wewe
kama wewe na kutaka mabadiliko. Hiyo tabia yako anza nayo, badilisha kauli zako
na tena uwe makini. Aga kabisa na usirudi tena kwenye ulevi, ugomvi usio maana.
Ishi maisha chanya na kutafuta mafanikio yako.
Acha
kuishi maisha yasiyokupeleka mbele kimafanikio. Penda maisha yako kwa kuishi
maisha ya faida siku zote. Jifunze pia kutunza muda wako. Acha kuangalia
angalia simu masaa yote wakati hakuna kikubwa unachokifanya huko. Ili kufanikiwa
kitu kikubwa unachotakiwa kwanza kukibadili ni wewe mwenyewe na si kitu
kingine.
Kumbuka
kama nilivyoanza kusema mabadiliko makubwa yaanzia kwako. Hapa ndipo mabadiliko
makubwa unayoyataka yanapoanzia. Utabaki kuona mabadiliko ya wenzako mpaka
lini? Yape maisha yako thamani kwa kuanza kubadilika kwanza na utaona karibu kila
kitu kinabadilika na kuwa na maisha ya tofauti. 
Post a Comment