Header Ads

VIDEO: Hatua nane zilizochukuliwa na serikali baada ya uhakiki wa mikopo ya wanafunzi


Wizara ya elimu, sayansi na teknolojia iliunda timu ya kuhakiki wanafunzi kwenye taasisi za elimu ya juu nchini ili kujiridhisha na uhalali wa wanafunzi wanaopata mikopo kwa ajili ya elimu ya juu. Baada ya uhakiki huo leo August 17 2016 Waziri wa elimu, Prof. Joyce Ndalichako ametoa taarifa ya zoezi la uhakiki wa wanafunzi wanufaika wa mikopo kwenye vyuo vya elimu ya juu nchini.
Katika taarifa hiyo imeeleza kuwa jumla wanafunzi 2,192 wanufaika mikopo katika vyuo 31 hawakujitokeza kuhakikiwa na wameigharimu serikali kiasi cha Bil 3.857.
Kutokana na mambo yaliyobainika Serikali imechukua hatua zifuatazo
  1. Vyuo vikuu ambavyo vimepokea fedha za wanafunzi ambao hawapo chuoni vinatakiwa virejeshe fedha hizo ndani ya siku saba kuanzia August 17 2016
  2. Vyuo vya elimu ya juu vinaagizwa kuweka mfumo mzuri wa uhifadhi wa kumbukumbu za wanafunzi kuanzia usajili, matokeo ya majaribio na ya mitihani na namba za akaunti za benki ambapo fedha za mikopo hilipwa.
  3. Vyuo vikuu vinaagizwa kuwasilisha bodi ya mikopo, kwa wakati taarifa zote za kitaaluma na za kibenki za wanafunzi ili kuiwezesha kufanya marekebisho stahiki katika kumbukumbu zao na kuepusha ulipaji wa fedha kwa wanafunzi wasiostahili.
  4. Bodi ya mikopo inapaswa kuchambua na kuingiza mara moja mabadiliko ya taarifa za wanafunzi kama zilivyopelekwa kutoka vyuoni ili kuepusha ulipaji wa fedha kwa wanafunzi wasiostahili.
  5. Hatua kali za kinidhamu zichukuliwe na kuingiza mara moja mabadiliko ya taarifa za waafunzi kama zilivyopokelewa kutoka vyuoni ili kuepusha ulipaji wa fedha kwa wanafunzi wasiostahili.
  6. Vyuo viweke utaratibu mzuri wa kudhibiti malipo kwa wanufaika wa mikopo ili kuepuka kufanya malipo kwa wanafunzi hewa.
  7. Wakuu wa vyuo ‘VCs’ na Principals’ waweke mfumo wa kuhakiki usahihi wa matokeo ya wanafunzi yanayotumwa bodi ya mikopo na watawajibika kwa usahihi wa taarifa zinazowasilishwa kwani zoezi la uhakiki limebaini kuwepo kwa usdadanganyifu mkubwa kwenye matokeo ya wanafunzi; wapo ambao hawakufanya mtihani au waliofeli lakini wameandikiwa PASS ili waendelee kupata mikopo.
  8. Uchunguzi zaidi utafanyika kwa miaka iliyopita ili kubaini fedha za mikopo ambzo zimelipwa kwa watu wasiostahili. Hatua hii inatokana na matokeo ya uchunguzi ambao umebaini kuwa wapo baadhi ya wanafunzi waliohitimu tangu mwaka 2013 lakini wameendelea kupokea fedha na wengine waliofukuzwa kwa kushindwa masomo tangu mwaka 2013/14 lakini bado wamelipwa hadi mwaka 2015/16.

ULIKOSA HII YA WIZARA YA ELIMU KUBAINI ‘MADUDU’ MIKOPO YA ELIMU YA JUU? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI


No comments

Contact us:Email:godfreymtega@gmail.com/WhatsApp-+255758297744/+255716824009 . Powered by Blogger.