VIDEO: Application iliyozinduliwa kwa ajili ya kuzuia ajali barabarani
Good news ni kwamba Jeshi la Polisi nchini kwa kushirikiana na kampuni ya Makini Road Safety Foundatini imeturahisishia njia nyepesi ya kukabiliana na ajali za barabarani ambapo kwa kutumia application ya MakiniApp ambayo ukiwa nayo katika simu yako inakusaidia kujua mwendokasi wa dereva kwenye gari ulilopanda.
Nakukutanisha msemaji mkuu wa MakiniApp Irene Kidunda…>>> ‘MakiniApp hii ni application ambayo inamuwezesha mtumiaji kufahamu kiwango halisi cha mwendokasi wakati anaoutumia dereva wakati wa safari kupitia simu yake‘
‘Ikiwa dereva anatembea kwa mwendokasi usiotakiwa mtumiaji anaweza kuchukua hiyo taarifa na kuituma katika kikosi cha usalama barabarani kupitia hiyohiyo simu yake ili askari wamchukulie hatua dereva huyo‘ –Irene Kidunda
‘Uzuri wa kuwa na application hii ni kwamba hatakama hutakuwa na mtandao kwa muda huo bado utakuwa na uwezo wa kurekodi mwendokasi wote na kisha ukampatia askari polisi utakayemkuta barabarani na bado ikawa na msaada‘ –Irene Kidunda
Kamanda wa Polisi kikosi cha usalama barabarani Mohamed Minga anasemaje kuhusu hatua hii?…>>>’Tumekuwa tukitoa namba ya simu ambayo abiria wataitumia kutoa taarifa za usalama barabarani ambazo ni 0682887722 na ukituma taarifa hizo sisi tunazifanyia kazi‘
‘Tunaamini mfumo huu wa MakiniAppy utatusaidia sana kudhibiti mwendokasi na kupunguza ajali za barabarani licha ya mfumo wa tochi tuliozoea kuutumia‘ –Mohamed Minga
Post a Comment