Header Ads

VIDEO: Aguero kakosa penati mbili lakini kawapiga hat-trick Dinamo Bucharest


Usiku wa August 16 2016 michezo 10 ya Play-Offs ya kuwania kucheza hatua ya Makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2016/2017 ilichezwa, miongoni mwa michezo iliyochezwa ni mchezo kati ya Manchester City dhidi ya Steaua Bucuresti.
374D272400000578-3743927-image-a-4_1471376280000
Katika mchezo huo uliyochezwa katika uwanja wa Nationala uliyopo Romania umemalizika kwa Man  City kuibuka na ushindi wa goli 5-0, miongoni mwa mastaa wa Man City waliofanya vizuri katika mchezo huo ni mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Sergio Aguero kukosa penati mbili lakini kufunga hat-trick.
374DE96A00000578-3743927-image-a-71_1471384550716

Man City wakiwa ugenini walifanikiwa kuanza kupata magoli kuanzia dakika ya 13 kupitia kwa David Silva, Sergio Aguero aliyefunga magoli matatu dakika ya 41, 78 na 89 ila goli la tatu lilifungwa na Nolito dakika ya 49, Man City watarudiana na Steaua Bucuresti August 24 katika uwanja wa Etihad jijini Manchester.


No comments

Contact us:Email:godfreymtega@gmail.com/WhatsApp-+255758297744/+255716824009 . Powered by Blogger.