Simba imemshusha Laudit Mavugo Dar es Salaam
Baada ya klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba kumuwinda kwa muda mrefu mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi aliyekuwa anaichezea klabu ya Vital’O ya kwaoBurundi Laudit Mavugo, hatimae usiku wa August 3 2016 aliwasili Dar es Salaam na kukabidhiwa jezi namba 45 akiwa uwanja wa ndege.
Mshambuliaji huyo aliyekuwa anawindwa na Simba kwa zaidi ya miaka miwili bila Simbakufanikiwa kumsajili, ametua Dar es Salaam baada ya kushindwa majaribio katika klabu ya daraja la pili Ufaransa, Laudit anaonekana kukubalika na kupewa nafasi kubwaSimba, tofauti na washambuliaji wengine wa kigeni ambao bado Simba inawajaribu.
Post a Comment