Header Ads

MICHEZO VIDEO: Chelsea wameanza kwa ushindi EPL dhidi ya West Ham msimu wa 2016/2017

Baada ya weekend ya August 13 na August 14 kuchezwa kwa jumla ya michezo 9 ya round ya kwanza ya Ligi Kuu England kuchezwa, usiku wa August 15 ilikuwa ni zamu ya klabu ya Chelsea chini ya kocha wao mpya Antonio Conte kuwakaribisha West Ham United katika uwanja wa Stamford Bridge.
3743D27700000578-3742126-image-a-82_1471291997444
Katika mchezo huo ambao wengi walikuwa wanamsubiria Antonio Conte kuona atafanya nini baada ya makocha wapya wenzake kama Jose Mourinho wa Man United na Pep Guardiola wa Man City kuibuka na ushindi katika michezo yao ya mwanzo wa msimu waEPL.
3744095F00000578-3742126-image-a-88_1471293810649
Chelsea wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1, Chelsea walianza kupata goli dakika ya 47 kwa mkwaju wa penati kupitia kwaEden Hazard ila James Collins alifanikiwa kuisawazishia West Ham dakika ya 77, uhakika wa Chelsea kuondoka na point tatu ulikamilika dakika ya 89 baada ya DiegoCosta kupachika goli la ushindi.
epl standing
Msimamo wa EPL baada ya mchezo wa leo August 15 2016


No comments

Contact us:Email:godfreymtega@gmail.com/WhatsApp-+255758297744/+255716824009 . Powered by Blogger.