Header Ads

JINSI YA KUTUMIA RASILIMALI ZA WENGINE KUJIONGEZEA KIPATO

                    Pesa sio kila kitu katika maisha, lakini inatusaidia sana katika kutupunguzia matatizo mbalimbali, ikiwa itatumiwa vizuri. Kuna wengi wanaofikiri kwamba hawastahili kuwa na pesa nyingi katika maisha yao. Lakini naamini kwamba wewe uko tofauti. Sababu kwa kusoma kwako makala hii, itakuwa inaonyesha kwamba; wewe ni mtu uliyeweka juhudi kubwa katika kubadilisha  maisha yako, yakiwemo ya kifedha. Nakupa pongezi kwa maamuzi unayoyafanya.

Hivi utachukuliaje kama nitakwambia kwamba; kutengeneza pesa kwa haraka ni rahisi? Nadhani utachukulia kuwa ni uongo. Si rahisi kupata pesa kwa haraka, lakini juhudi utakazoziweka katika kujitafutia kipato kamwe hazitopotea .Juhudi hizo ndizo zitakazokuja kukufanya kuwa na kipato cha kutosha hapo baadaye.

Ukiachana na hilo. Yakupasa utambue kwamba itakuwa ni rahisi kwako kujipatia pesa, ikiwa utafahamu mbinu na mipango sahihi utakayoweza kuitumia ili kupata pesa hizo. Kuna mbinu nyingi ambazo wengi wenye mafanikio wakiwemo matajiri wamekuwa wakizitumia katika kujiongezea kipato. Mbinu hizo ndizo zinazowafanya kila wakati waweze kujipatia pesa.

Na mojawapo kati ya mbinu hizo ni kutumia rasilimali za wengine. Wamekuwa wakitumia rasilimali za wengine kama vile muda, pesa, vipaji, ujuzi, na mtandao ili kujipatia pesa kwa haraka sana. Hiyo ndio siri ya kujipatia pesa kwa urahisi.


Usipoteze muda wako katika kujaribu kupata suluhisho juu ya tatizo fulani ikiwa kuna mtu mwenye ufunguo wa kutatua tatizo hilo. Kwa maana nyingine ni kwamba, usijaribu kujifanya kuwa mwenye akili sana, usijifanye kuwa ni smart au mvumbuzi kwenye  kila jambo.

Hivi ni sahihi kutumia rasilimali za wengine?

Ndio ni sahihi!! Ikiwa tu pande zote mbili zitakuwa zinanufaika. Unapotaka kuanza kutumia rasilimali za wengine hakikisha kwanza watu hao unaotumia rasilimali zao nao pia wanafaidika, na sio kuwatumia tu bila ya wao kupata chochote. Sioni sababu yoyote ya kwa nini usizitumie rasilimali zilizopo mbele yako.

Watu wengi wenye mafanikio wakiwemo matajiri wanakiita kitendo hicho cha kutumia rasilimali za wengine kuwa ni LEVERAGING. Hicho ni kitendo cha kutumia muda, pesa zako kidogo ili kujiletea matokeo makubwa. Baadhi ya matajiri wengi wanatumia siri hiyo katika maisha yao ili kujipatia pesa nyingi zaidi. Na kuna wanaotumia siri hii bila ya wenyewe kujua, na kuna wanaoitambua siri hiyo.

Na hata ukiwaangalia viongozi wengi wanaojihusisha na biashara ya mtandao utagundua kwamba nao wanatumia zaidi 'leverage', wanatumia rasilimali za watu kama vile muda na pesa ili waweze kujitengenezea pesa nyingi zaidi na wao kufanya kazi kwa muda mdogo. Tambua kwamba siri ya mafanikio ya kampuni yoyote inayojihusisha na biashara ya mtandao ni kutumia rasilimali za wengine. Na bila ya kufanya hivyo hakuna kampuni yeyote itakayoweza kufanikiwa.
Hata makampuni makubwa kama vile Nike, Dell , na makampuni yoyote yale. Kampuni zote hizo zinatumia  neno “leverage” kupitia wafanyakazi  wao ili kujipatia pesa nyingi zaidi.

Ili kujipatia pesa nyingi unatakiwa uelewe na ujifunze namna gani utaweza kutumia rasilimali za wengine ili kutengeneza hali ya ushindi kwa kila mtu. Na usipotumia leverage, utakuwa unauza muda wako kwa ajiri ya pesa. Na matokeo yake kila utakachoingiza kitakuwa ni kidogo ukilinganisha na kile unachokitoa. Na hicho hakitokuwa kitu kizuri ikiwa unataka kutengeza pesa kwa urahisi. Fikiria kutumia rasilimali za wengine  kwenye biashara yako hata kazi yako. Nakutakia kila la kheri.

No comments

Contact us:Email:godfreymtega@gmail.com/WhatsApp-+255758297744/+255716824009 . Powered by Blogger.