Binadamu wote tupo kwa kusudi maalumu hapa Duniani, tatizo ni kwamba wengi wetu hatulijui hili hivyo hupelekea wengi kuishi maisha ambayo hatukutakiwa kuishi, kwa mfano ukimfuga simba kama wanyama wengine atazoea kuishi kama wanyama wengine, lakini kumbe hakupaswa kuishi vile. Na hii hutokea kwa sababu amezoea kuishi na kundi la wanyama wa kufugwa hivyo hata makali yake kama simba yatapungua. Wengi wetu tunaishi maisha ambayo siyo yetu kwa sababu ya watu wanaotuzunguka wanaweza wakawa ni marafiki, ndugu pamoja na jamaa zetu. Hawa watu siku zote wamekuwa wakituambia maneno ya kutukatisha tamaa kama huwezi, alishindwa fulani na maneno mengine ya kukatisha tamaa. Usiwasikilize, amini kuwa wewe ni simba wa polini na si wa kufugwa. Ambatana na watu wanaopenda mafanikio (simba wenzako wa porini) na uache kuambatana na watu wasiopenda mafanikio (wanyama wa kufugwa) kwa sababu utakuwa/utaonekana kama wao.
Kumbuka: Kadri unavyopunguza uhusiano na baadhi ya kundi la watu, ndipo unapozidi kusogea kwenye mafanikio.
Usiambatane na watu ambao hawana faida kwako.
Mungu akumumba binadamu kuwa mnyonge duniani, mtegemee na umwamini yeye na pia fanya kazi kwa bidii
Post a Comment