Header Ads

WENGI TUNANUNUA VITABU VIDOGO VYA KUMBUKUMBU(DIARY) LAKINI HATUVITUMII.MALIZA MWAKA NA SOMO HILI

                            Kanune kitabu kidogo cha kuandika kumbukumbu alafu ukurasa wa kwanza andika taarifa zako za muhimu.Hata kama ikipotea ni rahisi muhusika kukurudishia.
ukurasa wa mwanzo andika mambo ambayo unahisi wewe yanakupa furaha
Ukurasa unaofuata andika mambo yanayokuhuzunisha 
Katikati mwa kitabu(diary) yako andika malengo yako yote kwa mwaka mzima iwe madogo au makubwa watu wengi tunatabia ya kuandika malengo makubwa tu na kuyapuuza yale madogo wakati yale madogo ndo yananguvu zaidi unapoandika malengo yako unaweza ukayatenga,KIROHO
KIJAMII,KIUCHUMI,KISIASA

Na uandike ni jinsi gani utayafikia malengo yako...
Na kwenye kurasa nyingine kila ukipata wazo lolote we liandike kwenye kitabu(diary) chako utashangaa wewe mwenyewe mwaka wako utakavyokuwa wa mafanikio.
Kurasa za nyuma andika matumizi yako na mapato itakurahisishia mambo mengi.
Note:unavyoandika andika kwa namna hata kitabu chako kikipotea siyo rahisi mtu kuelewa kwa haraka.Asanteni sana

NAWATAKIA HERI NA FANAKA YA SHAMU SHAMU ZA KRISIMASI NA MWAKA MPYA 
TULIANZA NA MUNGU TUNAMALIZA NA MUNGU !

No comments

Contact us:Email:godfreymtega@gmail.com/WhatsApp-+255758297744/+255716824009 . Powered by Blogger.