KILIMO BORA CHA VITUNGUU MAJI
Vitunguu ni zao la pili ambalo hutumika karibu katika mlo wa familia za kitanzania, Afrika mashariki na Dunia nzima.
Vitunguu vina chukua nafasi kubwa katika matumizi ya mboga hasa kwa wakazi wa mijini. Vitunguu hutumika katika kutengeneza kachumbari,kiungo cha mboga, nyama na samaki. Majani ya kitunguu pia hutumika kutengenezea supu n.k
AINA ZA VITUNGUU MAJI
Aina bora za vitunguu ni pamoja na Hybrid F1, Red creole na Bombay Red. Hizi ni mbegu bora ambazo zinatoa mazao mengi kuanzia 40kgs mpaka 60kgs kwa hekta.Mbegu bora katika zao la kitunguu ni Neptune F1, Jambar F1 pamoja na Rosset F1..Mbegu bora za vitunguu unawea kuzipata katika makampuni binafsi kama ya Kibo seed, Rotan seed, East Afrika seed company na kampuni za Balton na MASANTO katika kitengo cha mbegu. Pia unaweza kuzipata kwa wasambazaji wa mbegu pamoa na maduka ya TFA na maduka ya pembejeo za kilimo katika maduka mbalimbali.
UBORA WA MBEGU ZA VITUNGUUU MAJI
Ubora wa mbegu ni muhimu sana, kwani ndiyo chanzo cha mazao bora. Mbegu bora inatoa miche yenye afya na kuzaa mazao mengi na bora. Mbegu za vitunguu inapoteza uoto wake upesi baada ya kuvunwa (mwaka mmoja). Mbegu nzuri zina sifa zifuatazo :
Uotaji zaidi ya 80%, mbegu safi zisizo na mchanganyiko, zimefumgwa vizuri kwenye vyombo visivyopitisha hewa na unyevu. Hivyo mkulima anaponunua mbegu za vitunguu azingatie yafuatayo; chanzo cha mbegu, tarehe ya uzalishaji na kifungashio cha mbegu.
NB:Inashauriwa mkulima asipande mbegu zenye umri zaidi ya mwaka mmoja.
MAHITAJI MUHIMU KATIKA KUZALISHA ZAO LA VITUNGUU
Zao la kitunguu hustawi vizuri kwenye maeneo yasiyo na mvua nyingi sana,yenye baridi kiasi wakati wa kiangazi na yasiyo na joto kali pamoja na ufukuto wa ukungu wakati wa kukomaaa vitunguu.
Zao la vitunguu hustawi vizuri kwenye udongo wenye rutuba ya kutosha. Udongo unao ruhusu mizizi kupenya kirahisi, unao hifadhi unyevu kama vile udongo wa mfinyazi tifutifu.
NAMNA YA KUTAAYARISHA SHAMBA
Shamba liwe karibu na chanzo cha maji kwa ajili ya umwagiliaji. Matuta 1m X 3m au majaruba ya 2m X3m yanafaa kwa kupanda miche. Matuta au majaruba yanarahisigha umwagiliaji, palizi na kunyuzizia dawa. Upandaji wa mstari, mbegu hupandwa katika nafasi ya 1cm hadi 15cm kati ya mstari na mstari. Baada ya kupanda mbegu hufunikwa kwa udongo na baadaye kwa kuweka matandazo juu ya tuta. Mara baada ya mbegu kuota, matandazo yaondolewe na badala yake kichanja cha nyasi kijengwe ili kuiwekea kivuli mimea michanga.Mbegu ya kitunguu inachukua wastani wa siku 10 mpaka 14 kuwa yote imetoka katika hatua ya kitalu. Na haitakiwi izidishe siku 35 ambazo ni sawa na mwezi 1 na wiki 1 uwe tayari umeshahamisha kwenye shamba.
MATUNZO YA BUSTANI YA VITUNGUU
Umwagiliaji
Zao la vitunguu linahitaji maji ya kutosha katika kipindi chote cha ukuaji wa mmea na hasa wakati wa kutunga tunguu. Katika kipindi kisicho na mvua (mwezi mei hadi Agosti). Umwagiliaji ufanyika mara moja kwa wiki kwa udongo wa mfinyanzi tifutifu na vitunguu vilivyopandwa katika vijaruba. Ili kuharakisha kukomaa kwa vitunguu, unashauriwa kupunguza kiasi cha maji ya kumwagilia taratibu kadri zao linavyokuwa.
Hali ya hewa na maji ni vipengele muhimu sana vya kuzingatia katika uzalishaji wa vitunguu. Vitunguu vinastawi vizuri katika hali ya uakavu kwa kutumia umwagiliaji majia mengi sana lakini wakati wa masika inasababisha magonjwa mengi shasa ukungu,vitunguu haviwezi kukomaa vizuri,hivo kusababisha upotevu mkubwa wa mazao. Jua na hewa kavu ni muhimu sana wakati wa kukomaa na kuvuna vitunguu..
Pia ni vizuri uache kumwagilia maji mapema wiki nne hadi sita kabla ya kuvuna kwani muda kamili wa kukomaa na kuvuna kwa vitunguu ni siku 90 hadi 150 kutegemea na aina ya mbegu.
KUDHIBITI MAGUGU NA KUPANDASHIA UDONGO
Kitunguu ni zao lisiloweza kushindana na magugu. Magugu husababisha kupungua kwa ukubwa wa kitunguu, hueneza magonjwa na kusababisha kudumaa kwa vitunguu. Katika bustani ya vitunguu, magugu yanaweza kutolewa kwa njia ya kutifulia kwa jembe dogo, kung’olea kwa mkono na pia kwa kutumia madawa ya kuua magugu.
Kama unaondoa magugu kwa kutifulia, epuka kutifua kwa kina kirefu ili kutoharibu mizizi na vitunguu vyenyewe, kwani mizizi ya vitunguu ipo juu sana. Kupandishia udogo kwenye mashina ya vitunguu ni hatua muhimu ili vitunguu visiunguzwe na jua . Hakikisha kuwa mashina ya vitunguu yako ndani ya udongo kama sentimeta 5. Pia kuna aina ya vitunguu ambavyo hutoa au hupandisha tunguu lake juu ya udongo wakati vinapokuwa. Hivyo kupandishia udongo ili kufunika tunguu ni muhimu sana.
Katika hatua ya kitalu huwa kunatokea magonjwa ya ukungu (kata kiuno pamoja na barafu). Pia kuna wadudu wenye sifa ya kufyonza na kutoboa na pia wadudu wenye sifa ya usambazaji wa magonjwa ya virusi.(Inzi weupe ,vimamba,matobozi,vidukari na kadhalika)
Hivyo wakati huo utatumia dawa aina ya Ridomil Gold kwa kupambana na magonjwa ya ukungu kwa kipimo cha gram 50 kwa maji ya lita 20
Pia utatumia dawa aina ya Actara au Evisect kwa kupambana na wadudu kwa kipimo cha gram 8 kwa maji ya lita 20.
MATUMIZI YA MBOLEA
UUZAJI
Vitunguu ni zao lenye bei nzuri ukilinganishwa na mazao mengine ya mbogamboga na huuzwa kwenye masoko ya kawaida kwa bei nzuri.Kwani hivi sasa bei ya chini kabisa ya vitunguu kilo moja ni Tsh 1500= kama vitunguu vikilimwa vizuri na kuhudumiwa ipasavyo. Ekari moja huzaa gunia 70-90 sawa na kg 7000-9000. Kama ukipata soko la uhakika mkulima anaweza kupata hadi 13.5million kwa msimu mmoja.
Ndugu mkulima anza sasa kwa kulima kilimo cha vitanguu uone mafanikio.
NIKUTAKIE KAZI NJEMA
KWA MAWASILIANO
0754407774
Post a Comment