JINSI YA KUSAFISHA KEYBOARD YA KOMPYUTA!
Ngoja kwanza, hivi umeshawahi kufikiria kusafisha Keyboard ya kompyuta yako? Kumbuka unatumia muda mwingi sana kuobofya na saa nyingine hata hujali kama mikono yako ni michafu.
Ni vyema kusafisha Keyboard za kompyuta zetu mara kwa mara. Inapendekezwa kuzisafisha angalau mara mbili kwa mwezi.
Usafi kwa kifaa chochote cha kielektroniki ni muhimu sana. Usafi kwa kiasi Fulani ndio unaofanya vifaa hivyo vidumu kwa muda mrefu bila ya kuharibika au kupata hitilafu
Sasa basi ni njia gani nzuri ambazo unaweza tumia katika kuhakikisha unasafisha keyboard ya kompyuta yako bila ya kuiharibu?
Sasa basi ni njia gani nzuri ambazo unaweza tumia katika kuhakikisha unasafisha keyboard ya kompyuta yako bila ya kuiharibu?
Ili kujua Njia Hizo Fuata Vizuri Nyendo Hizi
>1. Kitu cha kwanza kabisa cha muhimu cha kufanya ni kuhakikisha kuwa unaitoa
keyboard hiyo kwa kuitenganisha na kompyuta (kama unatumia Desktop). Kama unatumia Laptop hakikisha tuu Laptop imezima kabisa na umetoa betri na haujaichomeka katika chanzo cha umeme.
>2. Tumia nguo yenye kitambaa laini kabisa kama vile kitambaa kilichotengenezwa kwa kutumia mali ghafi za pamba (kiwe laini kabisa). Saa nyingine kunakuwaga na vitaambaa spesheli vya kazi hii nakwa namna moja au nyingine huwa vinafanana na kitambaa kile cha kufutia miwani.
Ukitumia nguo au kitambaa kigumu hapa italeta shida kidogo maana unaweza ukaharibu kibonyezo kabisa kama sio kufanya maandishi ya herufi husika ya kibonyezo yakafutika. Na pia ni vyema kutotumia kemikali ya aina yeyote hapa
>3. Ukifikia katika hatua ya kuondoa uchafu mgumu mgumu ambao umeganda kidogo kati kati ya kibonyezo na kibonyezo unaweza ukatumia mswaki mkavu na ufute kwa utaratibu wa hali ya juu
>4. Ili kuhakikisha unatoa vumbi unaweza utatumia hewa yenye presha kubwa iliyohifadhiwa katika kopo. Hewa hiyo inakuwa na presha kubwa kiasi cha kwamba wakati inatoka inaweza ikasambaratisha vumbi. Kama huwezi kupata hewa hiyo basi huna budi kugeuza keyboard yako chini na kisha na kisha itikise kwa usarahu huku unabonyeza vibonyezo taratibu.
Post a Comment