Header Ads

WATANZANIA TUJIHADHARI NA UTAPELI UNAOSAMBAA MITANDAONI, HUU NDIO UKWELI KUHUSU WIZI HUO.

Baada ya kupigiwa simu na watu mbalimbali wakihitaji kujua uhakika wa pesa inayotangazwa kwenye mitandao ya OnlineTaskyPay, Money4Task na sasa Youthnize,MTEGA BLOG tumetafuta ukweli kuhusu hili.
 Kama ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii utakuwa tayari umeshakutana na post hasa kwenye mitandao ya WhatsApp inayokutaka ubonyeze link fulani ili ujipatie hela. Unapojisajili tu unapewa Dola25 ambayo kwa Tanzania ni takribani Elfu 60 kitu mabacho watu wengi wamekuwa wakijiingiza huko bila hata kujua hatma yake.
 Kwa uhakika mitandao hiyo ni ya uongo na ya kitapeli. Malengo ya mitandao ya namna hiyo ni kukupotezea muda, kuwatangaza wafahamike na hatmae kukuibia taarifa zako kama za anuani, barua pepe yaani e-mail na taarifa nyinginezo za kisiri.
Kwa nini mitandao hii ni ya uongo?
1. Hakuna usalama wa kutosha kwa mtumiaji, mtu unajisajili kwa dakika 1 na taarifa zako ni email, username na jina la hundi (Cheque), kitu ambacho hakiwezekani kwa miamala ya kifedha.
2. Mtandao unohusika huwa ni mmoja tu ambao huwa unatumia majina tofauti tofauti mfano mwanzoni ulianza na jina la OnlineTaskPay, baadae ukabadilishwa na kuwa Money4Task na sasa unajulikana kama Youthnize.
3. Ukishafikisha $300 na kuendelea utahitajika uthibitishe kama wewe siyo roboti kw akubonyeza link fulani mbapo link hiyo haifunguki kamwe.
4. Malipo yote wanayatangaza kuwa hutolewa kuanzia tarehe 24-30 na usipofungua akaunti yako kwa siku 30 akaunti yako inafungwa. Muda huo wa malipo ukifika huwa wanabadilisha jina kama ambavyo nimeeleza hapo juu.
5. Muundo wa Mtandao yaani Dashboard au Homepage ina taarifa za aina moja na ndiyo ushahidi wakusema kuwa mtandao huo ni mmoja mabao unabadilishwha jina tu.Unawea kutazama picha kwa ushahidi zaidi wa mtandao huu.

Huu ndio ukurasa wa mwanzo wa mtandao huo ninaouzingumzia. Matumizi ya ukuraza huu yalikuwa ni kwa mwezi wa 8 kuelekea wa 9. Anglia kwa makini muonekano wa homepage hii.

Baada ya kufikia mwezi wa 9 kuelekea mwezi wa 10 Mtandao huo ulibadilisha jina lakini hawakubadilisha homepage yaani muonekano wa ukurasa wa mwanzo. Mwanzoni waliita OnlineTaskPay, hapo chini walibadilisha wakiita Money4Task. Tazam picha hapo chini.


Baada ya kufikia mwezi wa 9 mwishoni sasa wamebdalisha jina na kuuita mtandao huu Youthnize ambapo muonekano wa mtandao huu ni wa aina ile ile kama ambavyo unaweza kuona kwenye picha hapo chini.
Huu ndio mpya unaoitwa Youthnize.

Kama unahitaji kuangalia kwa undani zaidi kuhusu mtandao huu unaweza kuutembelea kwa kubonyeza link hii hapo mbele ==>>>http://Youthnize.com/?ref=330296 kisha fuata maelkezo. Utajisajili kisha utapewa Dola 25 ndani ya sekunde kama 50 hivi tu. Kibaya zaidi unaweza kuona picha iliyopo chini mwa kila Homepage inayoeleza njia za ulipaji pesa ambazo ni PayPal, PayZa, MoneyGram na Cheque.


images/wu.jpg

Your Payment Withdrawal Option will appear here, when you will reach you minimum payout limit of 300$

You need [ 275 $ ] to get payout request form


Kumbuka unapojisajili unatakiwa kuweka Email yako na hiyo ndiyo inyotumika kudukua taarifa zako ambapo ni rahisi hata kukuibia endapo baadae utaambiwa utoe namba yak oya bank ili wakutumie hela.

Katika hali ya kawaida siyo rahisi fedh aikapatikana kirahisi kiasi cha namna hii. tufanye kazi Watanzania tusilimbuke na mitandao ya kijamii. Kwa ushauri kuhusu masuala ya mitandao usisite kuwasiliana nasi 0758297744.

MAELEKEZO YAO YAKO HIVI

Member Guide:
How do I promote my referral link?
Promote your referral link on forums, blogs, comments, chat rooms, chats, facebook wall, facebook pages, groups, twitter, ptc sites, advertising websites to get link visits and earn money on every visit you sent through your link

When will I get paid?
The minimum balance required for payout is 300$ and you can get paid through PayPal, Cheque, Western Union, Money Gram, bank transfer at end of every month.

How much can I earn?
You can earn without any limits, it depends solely on your efforts and how much you work to promote your link. Many of our top members are earning more then 200$ per day and 5,000$+ per month

This can't be real. Are you giving free money?
No, we are not giving away free money. We are paying you in order to generate traffic to our advertiser's websites. We will get paid from our advertisers for the traffic we bring to them and paid commission to you people.
Anti-CheatPlease note that we have a strong anti-cheat system, so do not bother sending fake traffic. You will get credited about it, but eventually you will not get paid and your account will get banned. Only send real people from real pages.
Note: Please note that if you have not logged in to your account for more than 30 days, all your earnings will be lost.
Source:jumaclick blog

No comments

Contact us:Email:godfreymtega@gmail.com/WhatsApp-+255758297744/+255716824009 . Powered by Blogger.