Header Ads

NJIA ZA KUIFANYA SIMU YAKO YA SMARTPHONE IJAE CHAJI HARAKA


Karibu ndugu msomaji wa makala hizi pendwa za technolojia kuhusu simu na computer zetu.MTEGA BLOG kuna wakati aliielezea makala hii kwa kutumia njia moja ya kuweka simu yako katika Aeroplane mode ili ijae chaji haraka. Ni njia sahihi na nzuri kwa sababu hata mimi naitumia kuchaji simu yangu mara nyingi Lakini kuna njia nyingine nyingi za kuifanya simu yako ijae chaji haraka. Sasa hizi ni baadhi ya hizo njia
1. IZIME SIMU YAKO UNAPOICHAJI
Ukizima simu unafanya shughuli zote zilizomo ndani ya simu zisimame yaan zile applications zinazofanya kazi chini kwa chini. Kwa hiyo matumizi ya betri yanakuwa 0% na hivyo kuifanya simu yako ijae chaji haraka

2. ZIMA DATA,BLUETOOTH,WIFI NA GPS
Hivyo vyote vikiwa ON au kimojawapo, hutumia nguvu betri kwa asilimia kubwa.Kwa mfano kama ukiwasha data utaendelea kupokea notifications mbalimbali mfano jumbe za Gmail au Whatsapp Hivyo ukizima unaipunguzia simu mzigo.Hiyo itakuwezesha kuichaji simu yako kwa haraka zaidi kwani shughuli zote za kutumia data zitakua OFF.

3.TUMIA KUCHAJIA CHAJA ORIGINAL
Hizi simu huwa zinaletwa na vifaa vyake original kama chaja.Kwa hiyo jitahidi unaponunua simu ununue na chaja yake ambayo imetengenezwa maalum kwa ajili ya hiyo simu.Usipende kutumia chaja zingine ambazo pengine ni bei rahisi na mara nyingi huwa zinaifanya simu inajaa taratibu sana na pengine haijai kabisa hata unachaji siku nzima.

4. USIICHAJI SIMU YAKO KWA KUTUMIA COMPUTER,DEKI AU LAPTOP
Najua utashangaa pengine kwa kuwa umezoea kuona watu wanachaji simu zao kwenye kompyuta,deki za dvd au laptop.Ukweli ni kwamba, yale matundu yote ya USB (USB ports) yamewekwa mahsusi kuweza kupitisha umeme kiasi cha 5V @ 0.5 amp.Kwa hiyo hicho ni nusu ya kiwango cha umeme unaotakiwa kuchaji simu.Maana yake ni kwamba simu yako itakuwa inaingiza chaji kwa nusu spidi ya ile ya kawaida kwasababu umeme unaoingia toka kwenye kompyuta ni nusu ya ule unaotakiwa.Na hii kwa namna moja ama nyingine  inaua simu. Hivyo nakushauri utumie chaji za kawaida ambazo zmetengenezwa maalum kwa simu.

5. USITUMIE SIMU YAKO WAKATI UNACHAJI
Pengine umeambiwa mara kadhaa au umesikia kuwa simu huwa zinalipuka ukiitumia huku unachaji.Ukweli ni kwamba haijathibitishwa, ila inategemea na ubora wa vifaa unavyotumia.Umeme ni umeme,kama vifaa unavyotumia ni fake,basi lolote linaweza kutokea.Sasa ukiwa unatumia simu huku unachaji itakuwa inaingiza umeme kiasi na kutoa kiasi.Kwa hiyo utatumia muda mrefu kuifanya simu yako ijae. Na kwa tahadhari tu usiongee na mtu ktk simu huku simu iko chaji.
UMEIPENDA MAKALA HII,TOA MAONI YAKO NA UTUAMBIE UNAPENDA TUANDIKE MAKALA KUHUSU NINI.

No comments

Contact us:Email:godfreymtega@gmail.com/WhatsApp-+255758297744/+255716824009 . Powered by Blogger.