FAHAMU JINSI YA KUSET INTERNET KWENYE SIMU YA ANDROID.
Ulishawahi kununua simu ukaweka lain lakini ikakataa kusoma data au ulishawahi kurestore simu ikakataa kusoma internet baada ya kuwaka lakini kabla ilikuwa inasoma data tena 3g? sasa ngoja nikwambie kitu>>>
Ili simu za android ziweze kusoma mtandao wa internet ninlazima zifanyiwe setting za kuziwezesha kusoma mtandao wa internet. setting hizo hujulikana kama access point. hivyo kama simu yako haina hizo access point haiwezi kusoma mtandao wa internet hata kama una kifurushi cha internet labda kama hizo access point zitaingia aoutomatic kutoka kwa ISP (INTERNET SERVICE PROVIDER mfano TIGO,VODA, AIRTEL n.k) wako.
Hivyo leo nitakuelekeza kutengeneza access point yako ambayo itakuwezesha kutumia internet kwenye simu yako kupitia lain yoyote ambayo utakuwa umejiunga kifurushi.
SASA FATA HATUA HIZI ILI KUTENGENEZA ACCESS POINT KWENYE SIMU YAKO
HATUA YA 1
fumgua menu ya simu yako ya android kisha nenda kwenye setting
HATUA YA 2
Baada ya hapo nenda palipo andikwa wireless & network, ukisha kuwa hapo bonyeza neno more
HATUA YA 3
Kisha bonyeza neno MOBILE NETWORKS
HATUA YA 4
Kisha bonyeza ACCESS POINT NAME
HATUA YA 5
Bonyeza menu ya simu yako ( hii inatofautiana kulingana na simuila utaitambua kwakuwa huwa na alama ya mistari mitatu chini kwa simu yako kulia au kushoto, au huwa imeandiwa kabisa kwa baadhi ya simu au huwa ni vidot vitatu kwa baadhi ya simu juu ya display upande wa kulia au kushoto juu)
boyeza hapo kisha chagua neno New APN.
ikifunguka itakuwa kama hivi
SASA FATA HATUA HIZI TENA
a. NAME
kwemye jina andika jina lolote hata la kwako
b. APN
kwenye APN hapo andika neno "internet"
c. APN type
kwenye APN type chagua "default" au kama kiboksi kinataka uandike wewe andika neno "default"
d. Proxy,port,username,password,server,MMSC,MMS proxy,MMS port
hivi achana navyo kwani havina umuhimu.
e. Authentication type
hapo chagua PAP au chagua PAP or CHAP
f. APN Protocal
hapo chagua IPV4 au chagua IPV4 or IPV6
g. Bearer au Data bearer
chagua "unspecified"
ukimaliza kujaza hapo bonyeza tena menu ya simu yako kisha bonyeza neno save, na hapo utakuwa tayari umeshatengeneza access point yako ambayo itakuwezesha kutumia internet kwenye simu yako ya Android.
Sasa rudi mwanzo kabisa wa simu yako kisha nenda sehemu ya kuwezesha data kisha wezesha hiyo data angalia kama itasoma ( itaanza kusoma E na kisha 3G) kama ina sapoti 3G na itasoma E kama haisapoti 3G
Ili simu yako iweze kushika data vizuri iweke kwenye flight mode kwa muda wa sekunde kumi kisha itoe kwenye flight mode.
Sasa furahia huduma ya internet kwenye simu yako>>>>>
Post a Comment