TOFAUTI KATI YA WEBSITE NA BLOG
Tofauti
kati ya Blog na Website imekuwa ikichanganya sana hasahasa kipindi hiki ambacho
utasikia sana neno Blog. Lakini je umeshawahi kujiuliza kuna tofauti gani kati
ya website na blog?
Kwa kifupi
ni kwamba blog ni aina ya website ambayo inajulikana kama Web Log na
kuchukuliwa herufi ya mwisho ya Web ambayo ni "b” na kuunganishwa na neno zima
la mwisho ambalo ni Log na kuwa Blog. Unaweza kuwa umeshawahi kusikia kuhusu
Static and Dynamic websites.
Blog
inaweza kuwa ndani ya website au inaweza pia kujitegemea yenyewe kama yenyewe. Ikiwa
una website basi unaweza ndani yake ukaongeza blog. Na blog haiwezi kabisa kuwa
website.
Kutokana na
Wikipedia, Blog ni sehemu ya website ambayo ina taarifa zenye kuongezwa na
kubadilishwa kila siku huku kukiwa na nafasi ya watembeleaji kuweka maoni yao
juu ya mada unazoandika humo.
TUNATENGENEZA BLOG NZURI KUANZIA Tsh 20,000/= na ANDROID APPLICATION YAKE NI Tsh 30,000/= 0758297744/0716824009
TUNATENGENEZA BLOG NZURI KUANZIA Tsh 20,000/= na ANDROID APPLICATION YAKE NI Tsh 30,000/= 0758297744/0716824009
Blog huwa
mara nyingi zina taarifa nyingi mbalimbali na huwa mpya (up to date) kila siku
kwani mwenye blog anakuwa akiongeza taarifa kila siku au kwa muda maalum. Na lugha
inayotumika sanasana inakuwa ni rahisi na yenye kueleweka na pia taarifa zake
ni rahisi kuzitafuta kwani huonekana katika Blog Achieve.
Katika Blog
kuna kitu kinaitwa vipachiko (Posts). Kila post ina page yake inayojitegemea Lakini
page kuu (main/ home page) ya blog inakuwa ina muhtasari wa mada za karibuni za
Blog hiyo na kila mwisho wa mukhtasari utaona neno Read More ambapo ukibofya
hapo ndiyo inakupeleka katika ukurasa maalum wa mada hiyo peke yake.
Kitu kingine
ni kwamba, katika blog huhitaji kutengeneza ukurasa kwaajili ya mada unayotaka
kuanzisha bali kurasa hujitengeneza automatically pale tu unapoandika mada mpya
na kuisave, Lakini katika website ukitaka kuanzisha mada inabidi kwanza
utengeneze page yake kisha ndiyo uandike mada hiyo.
Kutokana na
ugumu huo ikiwa una website na unajua kwamba utahitaji kuwa na mada nyingi za
kuongeza kila muda basi ni vema ukaongeza Blog katika hiyo website ili
ikurahisishie kazi hiyo.
TUNATENGENEZA BLOG NZURI KUANZIA Tsh 20,000/= na ANDROID APPLICATION YAKE NI Tsh 30,000/= 0758297744/0716824009
TUNATENGENEZA BLOG NZURI KUANZIA Tsh 20,000/= na ANDROID APPLICATION YAKE NI Tsh 30,000/= 0758297744/0716824009
Mara nyingi
website zinakuwa hazina taarifa nyingi sana na ndio maana nyingi zinakuwa
hazina Blog ndani yake, mfano wa website ambazo hazihitaji blog ni kama vile
website za vyuo, mashule, n.k kwani hakuna cha kuongeza kila siku zaidi ya
kurasa maalum tu ambazo zinakuelekeza jinsi ya kujiunga na chuo fulani, uongozi
wao, maabara, maktaba, ukurasa wa mawasiliano na kuhusu wao basi. Lakini website
zinazokuwa na blog ni kama za habari, tuition, na mafunzo mbalimbali kwani
utahitaji kila muda kuweka habari mpya au somo jipya.
Mara nyingi
website taarifa zake zinakuwa ni zilezile tu au hubadilika mara chache sana na
kama kuna jambo la kuongezeka basi hutokea kwa nadra sana au kwa kipindi
maalumu.
Zifuatazo ni
baadhi ya sifa za blog
- Ina sehemu ya kuacha maoni katika kila mada
- Inawekewa mada mpya mara kwa mara
- Search Engine kama vile google huitembelea mara kwa mara (Frequently crawled by Search engines) ili ijue mada mpya ulizoweka ili iweze kuziweka katika results zake pale mtu anapotafuta katika Google.
- Huwa na taarifa nyingi sana.
Kwa upande
wangu ni hayo tu, unaweza kuacha maoni yako hapa ikiwa una lolote la kuongeza.
KWA USHAURI WASILIANA NASI:075829744/0716824009
KWA USHAURI WASILIANA NASI:075829744/0716824009

Post a Comment