Header Ads

JIAJIRI KWA KUFUNGUA BLOG YAKO (JIUNGE NA GOOGLE ADSENSE)

Ndio unaweza kupata hela katika blogu yako kwa kutumia programu ya Google Adsense.
Google Adsense ni programu  ambayo inatumiwa na  wamiliki wa blogu na tovuti (Publishers), kuonyesha matangazo ya Google (Google Adwords)

Unachotakiwa kufanya ni kujisajili katika programu hii Google Adsense, wao wataikagua blogu yako na kama blogu yako au tovuti yako itakizi mahitaji yao basi watakupa kibali na namna ya kuweza wewe kuweka matangazo yao kwako.

Matangazo haya  ya Google Adsense yatakupa wewe hela kwa KUBOFWA (Clicks) na KUONEKANA (Impressions).


Angalizo
Hutakiwi Kubofya (Click) matangazo haya wewe mwenyewe. Acha watu wanaotembelea blogu au tovuti yako wabofye wao kwa mahitaji yao. Google Adsense wanayo namna ya kuangalia kama unafanya mchezo wa kubofya matangazo wewe mwenyewe na wakigundua hili hakuna onyo wanakufungia huduma hiyo.
Sasa ili uweze kupata Bofya (clicks) za kutosha pamoja na muonekano (Impressions) lazima blogu au Tovuti yako iwe na watembeleaji wa kutosha. Na namna ambavyo utapanga matangazo yako ili iwe na urahisi kwa watembeleaji kujionea matangazo kwa urahisi.

Kanuni ya iko hivi

WATEMBELEAJI WENGI + BOFYA ZA KUTOSHA = HELA ZA KUTOSHA

Nisikuchoshe kwa leo hadi wakati mwingine tena. Kwa maoni au maswali niandikie kwa barua pepe godfreymtega@gmail.com

No comments

Contact us:Email:godfreymtega@gmail.com/WhatsApp-+255758297744/+255716824009 . Powered by Blogger.