Serikali ya Marekani yatoa dola milioni 407 kwa Tanzania
Serikali ya Marekani jana Jumatatu imekubali kuipatia Tanzani zaidi ya dola za Marekani milioni 407 kama msaada.
Hii imekuja baada ya Marekani kukataa kutoa kiasi cha pesa kama hiki mwezi Machi mwaka huu kutokana na serikali ya Tanzania kushindwa kutimiza matakwa ya demokrasia.
Ubalozi wa Marekani umesema pesa hizo zimetolewa ili kusaidia Tanzania katika nyanja za afya, kilimo, elimu, utunzaji wa maliasili, nishati na utawala wa kidemokrasia.
''Hii ni nusu ya pesa ambazo Marekani inatarajia kuipatia serikali ya Tanzania kwa ajili ya maendeleo'', Ubalozi wa Marekani umesema.
Profesa wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Haji Semboja ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa huu msaada ni kielelezo kuwa serikali ya Marekani inakubaliana na kinachoendelea nchini katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii.
MAREKANI YAIPIGA JEKI TANZANIA SHILINGI BILIONI 895
Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Maendeleo la Marekani, USAID, Bi. Sharon Cromer, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile, wakitia saini Hati ya makubaliano ya msaada wa Zaidi ya shilingi Bilioni 895, kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka wa fedha 2016/2020, Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Maendeleo la Marekani, USAID, Bi. Sharon Cromer (Kushoto), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile, wakiwa wameshika Hati za makubaliano baada ya kukamilika kwa tukio la utiwaji saini makubaliano ya msaada wa Zaidi ya shilingi Bilioni 895, kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka wa fedha 2016/2020, Jijini Dar es salaam.
Kaimu Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Mamelta
Mutagwaba, wakiteta jambo na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la
Maendeleo la Marekani, USAID, Bi. Sharon Cromer (Katikati), baada ya
kukamilika kwa tukio la utiwaji saini makubaliano ya msaada wa zaidi ya
shilingi Bilioni 895, kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya
maendeleo hapa nchini katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia
mwaka wa fedha 2016/2020, Jijini Dar es salaam.
Na Benny Mwaipaja, MoFP, Dar es salaam
SERIKALI ya Marekani, kupitia shirika lake la Misaada ya Maendeleo USAID, imeipatia Tanzania msaada wa dola Milioni 407 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 895 zitakazotumika kwaajili ya kuendeleza sekta za Kilimo, Afya, Nishati ya Umeme, Elimu na Utawala Bora, katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka 2016/2020.
Hati za Makubaliano hayo zimetiwa saini Jijini Dar es salaam, kati ya Mkurugenzi wa Shirika la USAID, Bi. Sharon Cromer, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile.
Msaada huo ni sehemu ya dola Milioni 800, sawa na zaidi ya shilingi Trilion 1.76 ambazo serikali ya Marekani kupitia USAID, imepanga kuipatia Tanzania ili kufanikisha Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa katika kipindi cha miaka mitano ijayo, wenye lengo la kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo mwaka 2025.
Kiasi hicho cha fedha kitatumika na serikali ya Tanzania kupitia mfuko mkuu moja kwa moja wakati kiasi kingine kitatumiwa na Taasisi zisizokuwa za kiserikali zinazofanya shughuli zake hapa nchini kufanikisha malengo ya msaada huo.
Miradi iliyopewa kipaumbele ni pamoja na kupambana na UKIMWI na Kifua Kikuu, Uzazi wa Mpango, Kupunguza vifo vya mama na mtoto, kukuza utawala wa kidemokrasia, Usimamizi wa Rasilimali za Taifa, na kuwekeza kwenye sekta ya umeme ili kuimarisha sekta ya viwanda na uzalishaji mali.

Post a Comment