Header Ads

JINSI YA KUPATA MAFANIKIO KATIKA BLOGU AU TOVOTI


 
Naam ni wengi sana wamekuwa wakianzisha blog au tovuti na kuishia njiani bila kuona mafanikio. Hapa nitazungumzia mambo makuu ambayo kama ukizingatia basi utafanikiwa katika blogu yako au tovuti. Kuna mambo ya kuzingatia kabla ya kuamua kuanzisha blogu au tovuti yako.



  • MADA /TOPIC  ni swala la muhimu sana kuzingatia kabla hujaanzisha blogu au tovuti yako. Wengi  wemeshindwa kutoka na kutokujipanga katika swala hili. Kama unataka kuwa na blog kwa ajili ya habari basi uwe umejipanga vizuri katika kupata habari mpya na sio kunakili kutoka katika blog zingine za habari. Wadau wengi wanaanzisha blogu ila hawaoni mafanikio kwa vile hawana kitu cha kuvuta wadau katika blogu zao.
·         8020fashions ni moja ya blog ambayo imefanikiwa sana hapa Tanzania, mwanadada huyo yeye amejikita katika mambo ya wanawake. Hachanganyi mambo.

·         Issamichuzi  pia ni blog yenye mafanikio makubwa sana kwa vile yeye ni mwanahabari na blog yake ni ya habari. Wengi mnakosea kwa vile mnaanzisha blog za habari ila hamtafuti habari bali mnanakili kutoka kwake
  • PATA MUDA wa kutosha katika kushughulia blogu yako ili kuweza kuyaona mafanikio. Wengi wanakata tamaa mapema kwa vile hutaka mafanikio ya haraka sana katika blogu na tovuti.
  • JITANGAZE , kuna namna nyingi za kuweza kuitangaza blogu yako na kufanya ifahamike na wengi. Unaweza fanya link exchange kutoka kwa watu wengine wenye blogs. Ni kuwa unaweka link zao kwako na wewe unawaomba waweke link yako kwako.  Vile vile waweza inadi blog yako kwa njia ya radio, google adwords. Mada hii ni ndefu sana ya namna ya kuinadi blog yako. Endelea kutembelea blog hii nami nitakuwa naleta mada mbali mbali za kukusaidia katika kuinadi blog yako.
  • MATANGAZO, kama utaweza kuvutia watangazaji katika blog yako basi utakua umefanikiwa kwa kiasi kikubwa. Ila hili litawezekana kama ukizingatia mambo ambayo nimeyazungumzia hapo juu.

No comments

Contact us:Email:godfreymtega@gmail.com/WhatsApp-+255758297744/+255716824009 . Powered by Blogger.