FB INSTA TWITTER Tanzania yatajwa kati ya nchi zinazoongoza wahitimu elimu ya juu wasio na sifa Afrika Mashariki.

Moja habari zilizoandikwa ni hii ripoti kwenye gazeti la Jambo Leo yenye kichwa cha habari ‘Ripoti 61% wahitimu elimu ya juu ni vilaza’
Gazeti la Jambo Leo katika ukurasa wake wa mbele limeripoti ripoti kuhusu mtazamo wa waajjiri katika nchi za Afrika Mashariki iliyochapishwa mwaka juzi, katika ripoti hiyo imeonesha kuwa asilimia 61 ya wahitimu katika vyuo vya elimu ya juu Tanzania, hawana sifa za kushindana katika soko la ajira.
Hali hiyo kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyojumuishwa katika taarifa kuhusu usawa katika jamii ya Afrika Mashariki iliyotoka mwishoni mwa wiki iliyopita, imetilia shaka uwekezaji wa elimu ya juu, kwamba huenda uwekezaji wa pata potea.
Katika ripoti hiyo ya mtazamo wa waajiri iliyochapishwa mwaka juzi na Taasisi ya Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki (IUCEA) kwa kushirikiana na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC), imeeleza kuwa katika tatizo hilo katika nchi za Afrika Mashariki, Tanzania ni ya pili kwa kuwa na wahitimu hao wasio na sifa.
Nchi ya kwanza kwa mujibu wa ripoti hiyo kwa kuwa na wahitimu wa aina hiyo ni Uganda, ambayo imetajwa kuwa na asilimia 63 ya wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu, wasio na mbinu kuhusu soko la ajira.
Burundi imetajwa kuwa ya tatu baada ya Tanzania ambayo ina asilimia 55; Rwanda ya nne kwa kuwa na asilimia 52 na Kenya ikiwa na wahitimu wachache wa aina hiyo ambao hata hivyo ni asilimia 51 ya wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu.

Post a Comment