Maendeleo na Mafanikio
Habari ndugu mpenzi mfuatiliaji wa Blog yetu ya MTEGA BLOG, Moja kwa moja tuanze somo letu linalohusu Maendeleo na Mafanikio.
Maendeleo na
mafanikio ya mtu yanaletwa na
chuki aliyokuwa nayo juu ya maisha yake anayoishi, ili kuweza kufanikiwa
unaitaji kuwa na mawazo chanya juu ya kila utakalolifanya haijaishi una elimu
kiasi gani, ila mtazamo wako ndiyo utakaokuletea mafanikio yako. Usiwe na mawazo
mgando ukitegemea kitu kimoja tu maishani, kwa mfano watu wengi sasa hivi wanategemea
elimu ya darasani tu bila kuangalia na vitu vingine vitakavyowasaidia na ndiyo maana kila siku wanaishi maisha ya kawaida. Sikatai
wewe kuwa na elimu ya darasani, lahasha; bali unatakiwa pia kuwa na elimu
nyingine itakayokuwezesha kufikia malengo yako/ Elimu ya mtaani.
Watu wengi wanaotajirika siku
hizi ni watu wanaotumia elimu mbadala katika maisha yao(Elimu ya mtaani),
wanafanya biashara, wanafungua makampuni na pia wanafanya kazi kwa bidii zote
kufikia ndoto zao. Kama umefeli darasani usikate tamaa bali ndo iwe hatua ya wewe
kuendelea mbele, kuwa kama wakina Billgate,Ben Carstol ambao wao pamoja
na kufeli masomo yao darasani hawakukata tamaa ndo maana hadi leo hii ni watu
wanaoheshimika sana na wenye hela. Pia kwa Tanzania tuna watu kama Erick
Shigongo ambao wamekuwa watu maarufu sana. Ila ukifuatilia histolia yake alikuwa
na maisha magumu sana aliyoanza nayo.
Jisemee mwenyewe kuwa; Mimi hata
kama nitashindwa kuendelea na masomo yangu ya chuo kikuu sitakata tamaa maana
najua hapo ndipo ushindi wangu utakapoanzia katika safari yangu. Nitahakikisha
naishi katika ndoto yangu ya kuja kuwa mtu maarufu Tanzania, Afrika na Dunia
nzima. Nitautumia uchungu wa kufeli katika kujiletea maendeleo yangu na familia
yangu. Nitahakikisha nakuwa na familia iliyo bora, yenye kila kitu. Nitamiliki
nyumba ya ndoto yangu, magari ya ndoto yangu kama Ferrari, Aston malt,
Lambogine, Buggat n.k.
Tuonane kesho katika sehemu ya pili na ya mwisho ya hii mada yetu. Asante kwa kutembelea Blog yetu na usisite kuendelea kutembelea mara kwa mara ili kupata vitu vizuri zaidi vitakavyo kujenga na kukuelimisha.

Post a Comment