Maendeleo na Mafanikio 2
Leo tunaendelea sehemu ya pili na ya mwisho ya somo letu hili la Maendeleo na Mafanikio
Mafanikio aliumbiwa mwanadamu ila
Shetani kutokana na wivu wake amekua akizuia mafanikio hayo asiyapate
mwanadamu, ndiomaana watu wanaishi maisha ya kimaskini pasipo kuelewa. Kama
usipotambua nafasi yako Mungu aliyokuwekea hakika utaendelea kunyanyaswa na Shetani
katika maisha yako. Ni vema ukabadilika na kukaa katika nafasi yako
aliyokuwekea Mungu kwa maana utajili una yeye Mungu wetu.
Kusudi la Mungu siyo wewe uishi
maisha ya kimaskini, watu wanaishi maisha magumu kwa kutotambua kusudi la Mungu
katika maisha yao. Hata neno la Mungu linasema; Fedha na dhahabu zote ni mali
ya Bwana. Fanya kazi kwa bidii pamoja na kumtumikia yeye hakika utaupata
utajili.
Marafiki ni muhimu katika maisha
ya mwanadamu kwa sababu wanaweza kutupa mawazo juu ya yale tunayowaza kuwa ni
mazuri au la! Na kwamba yanaweza kutusaidia vipi katika maendeleo yetu. Japokuwa
siyo marafiki wote wanaweza kutupa
mawazo ya maendeleo.
Remember:
- The less you associate with people the more your life improve also it is better to be alone than having a bad company
- You are responsible for your life
- The first witch of your success is you
- No one is coming to save you. This life of yours is 100% of your responsibility

Post a Comment