Header Ads

Kuzuia upotevu wa data zako muhimu ktk Computer.

Mpendwa mpenda kuelimika ktk teknolojia, hiki kitu hapa chini si chakupuuza hata kidogo kwani kitakusaidia kuongeza ufanisi ktk kazi zako binafsi na za kiofisi/kampuni.

Unapokuwa unafanya kazi nyingi kwa kutumia Computer na unaona wazi kuwa una vitu vya muhimu sana na pengine unaingiwa na wasiwasi kuwa endapo vikipotea au ikatokea Computer imepata tatizo la ghafla basi utapoteza kila kilicho cha muhimu, sasa basi kuepuka hayo fuata fomula hii ya utunzaji wa data;
Jina la fomula ni “tatu, mbili, moja” yaani (3-2-1)
Namna ya kutumia Fomula hii ni kama ifuatavyo;

Hatua ya kwanza,

  1. Kama una data zako za muhimu sana basi ziweke ktk folder moja, kisha hilo folder liandike jina utakalopenda wewe,
  2. Baada ya kuandika jina hilo ambalo pia ni rahisi kulikumbuka,
  3. Sasa tunaanza kutumia fomula yetu, na hapa tunaanza na ile namba 3 ya mwanzo, maana ya hiyo namba ni kwamba, hilo folder lako, unatakiwa kulitoa kopi mara mbili, yaani utengeneze kopi zake nyingine mbili, na KWA UJUMLA UWE NA MAFOLDER MATATU, (Folder Original, Kopi Ya Kwanza Ya Folder Original Na Kopi Ya Pili Ya  Folder Original)

Hatua ya pili,

  1. Hatua hii ni kuhusu namna ya kutunza mafolder yako yale mawili uliyotoa kopi (na hii ndio maana ya ile namba 2 kutoka kwenye fomula),
  2. Folder la kwanza tutalitunza ktk External hard disk au ktk flash disk,
  3. Folder la pili kama sio kubwa basi unaweza kulichoma kwenye Cd/dvd,
  4. Au kama folder la kwanza uliweka ktk External hard disk basi la pili weka ktk flah, na maana ya ile namba mbili kwenye fomula ni kwamba, TUNZA HIZO KOPI ZA MAFOLDER MAWILI KTK SEHEMU MBILI TOFAUTI.

Hatua ya tatu na ya mwisho,

  1. Hapa tunaongelea ile namba 1 ya mwisho kwenye fomula yetu,
  2. Maana ya hiyo namba moja ni kwamba baada ya kutunza kopi za mafolder yetu mawili sehemu mbili tofauti hatua inayofuata ni hii;
  3. Kitunzio kimoja chenye folder letu moja tunakipeleka sehemu nyingine tofauti kabisa na ile tunayofanyia kazi zetu,
  4. Yaani kwa mfano unafanya kazi ofisini kwako na umetunza kopi ya folder la kwanza ktk External hard disk, na kopi ya folder la pili katika flash, unatakiwa kuchukua kitunzio cha folder kimojawapo iwe ni hiyo hard disk au iwe ni hiyo flash au iwe ulizichoma kwenye CD/DVD na ukipeleke nyumbani kwako ukakiweke kabatini (ufiche kabisa), na kitunzio kingine kitakachobaki ukiache hata kwenye droo ya meza yako ya ofisi,
  5. Na maana halisi ya hiyo namba 1 kwenye fomula ni KUTUNZA KITUNZIO KIMOJA CHENYE KOPI YA FOLDER LAKO SEHEMU TOFAUTI NA UNAYOFANYIA KAZI, ili ikitokea kimoja kimeibiwa basi unakuwa na kingine sehemu nyingine ambayo mwizi au virus hawafahamu.
  6. Wataalamu wengi kama sisi hupenda kutunza folder hili moja ktk drives zilizo mitandaoni kama (Google Drive, One drive n.k)

Hitimisho;

Hii sio kwa watumishi wa Serikali au watu binafsi bali hata wanafunzi, na ukweli ni kwamba ukiweza kutumia fomula ya “tatumbilimoja” / “321” yaani (MAFOLDER MATATU “Original, kopi ya kwanza, kopi ya pili”MAFOLDER MAWILI KTK SEHEMU MBILI TOFAUTIKITUNZIO KIMOJA CHENYE KOPI YA FOLDER LAKO SEHEMU TOFAUTI NA UNAYOFANYIA KAZI) basi daima hautopotelewa na data zako nautakuwa tayari kuzirudishia muda wowote endapo zitaibiwa au kuvurugwa na wadudu/virus.

Angalizo;

Pale unapokuwa na ongezeko la data ktk Computer basi ziongezee pia ktk vitunzio vile viwili ili kuongeza ukamilifu wa data zako.c
Usisite kuwasiliana nasi kwa msaada zaidi(0758297744/0716824009)

No comments

Contact us:Email:godfreymtega@gmail.com/WhatsApp-+255758297744/+255716824009 . Powered by Blogger.