TIMU YA SERENGETI BOYS YAISHINDA MECHI YA KIRAFIKI DHIDI YA DYNAMO
Timu
ya Mpira wa Miguu ya vijana wa Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 17
‘Serengeti Boys’ imefanya kambi yake kwa mafanikio huko jijini Victoria
kwenye Kisiwa cha Mahe, nchini Shelisheli baada ya kuibuka na ushindi
wa bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya dhidi ya
Northern Dynamo.
Katika
mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Taifa wa Shelisheli, bao pekee la
Serengeti Boys lilifungwa na Muhsin Makame katika dakika 75 ya mchezo
huo uliokuwa na ushindani mkali katika vipindi vyote viwili kutokana na
kushambuliaana mara kwa mara.
Serengeti
Boys ambayo ilikuwa na kikosi cha nyota 21 na viongozi watano,
wamemaliza kambi ya huko Shelisheli na hivyo inaondoka jioni ya leo
Septemba 13, 2016 saa 11:00 jioni na ikitarajiwa kuingia nchini usiku wa
saa 7:45 Septemba 14, 2016 ambako itakuwa kambini hadi siku ya mchezo
Jumapili Septemba 18, mwaka huu.
Mchezo
huo wa kuwania kucheza fainali za kucheza fainali za Kombe la Mataifa
ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17. Fainali hizo
zitafanyika jijini Antananarivo, Madagascar hapo Aprili, 2017.
Kocha
Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Nyundo Shime maarufu kwa jina la Mchawi
Mweusi, amesema: “Sitaki kuwa na maneno mengi. Nataka Watanzania waje
kuona wenyewe. Maana maneno maneno yakizidi inakuwa kama kero. Nataka
kujenga utamaduni wa Watanzania kuja wenyewe uwanjani kuona timu yao.”
Katika
hatua nyingine, wapinzani wa Serengeti Boys wanatarajiwa kutua Alhamisi
wakiwa na kikosi cha watu 40 na kati ya hao ni 22 ni wachezaji.
Miongoni kwa kundi hilo pia kuna wanahabari wanne.
Katika
orodha ilitumwa TFF, wachezaji wa timu hiyo ni pamoja na Mathieu Lee
Valtair, Balou Prince Joel, Bopoumela Chardon, Kiba Konde Ridrique,
Kibasila Christ Benilde, Langa Lessen Bercy, Makouana Beni, Mantouari
Juste Aldo, Mata Thomas, Mbemba Patchely Rael, Mbenza Kamboleke,
Mboungou Prestige, Mebeza Egouep Craiche, Mouandza Mapata, Moungala
Ikounga, Mountou Edouard, Ngakosso oko Alves, Ngaloukossi Jossy Ronel,
Nguienda Mouanga Bernice, Nguimbi Exau, Ntoto Gedeon, Oboua Danish na
Otang Jeordon.
Viongozi
wa timu hiyo wamo Ntoto Lacombe ambaye ndiye Mkuu wa Msafara, Goma
Ambroise Stephane ambaye ni Mratibu wa msafara, Ngami Gobard – Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Congo – Brazzavile.
Wengine
ni maofisa mbalimbali Otende Charles, Moussavou Merrile, Badji Mombo,
Berrettini Paulo, Ekariki Basile, Cesana Eraldo, Bakoua Loufouma
Narcisse, Okandze Elenga Jean Pierre, Lounou Joste Feller, Mabila Kengue
Francois, Loemba Jean Rufin, Mendome Ndoum, Batangounna Ntari na Mbemba
Gervais.

Post a Comment