Rooney kaachwa katika kikosi cha Man United kitakachocheza na Feyenoord
Nahodha wa Man United Wayne Rooney
ameachwa katika kikosi cha Man United kilichosafiri kuelekea Uholanzi
kucheza mchezo wake wa kwanza wa Europa League dhidi ya Feyenoord, Jose
Mourinho amesafiri na kikosi cha wachezaji 20.
Stori kutoka katika tovuti rasmi ya Man
United inaeleza Man United kusafiri kwenda Uholanzi kwa ajili ya mchezo
na Feyenoord na wachezaji 20 tu ikiwa imewaacha wachezaji kama Antonio
Valencia, Jesse Lingard na Wayne Rooney licha ya kuwa walifanya mazoezi
na timu asubuhi.

Hakuna sababu rasmi iliyotolewa kuachwa
kwa nahodha huyo lakini kiungo Henrikh Mkhitaryan nae ameshindwa kufanya
mazoezi na timu kutokana na kuuguza jeraha lake la mguu na Phil Jones
hakufanya mazoezi na timu.
Post a Comment