RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 3 & 4
Mtunzi : EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
“Hakikisheni huyu dada nina lala naye usiku wa leo sawa”
Muntar
aliwaamrisha wapambe wake na wakamtii na mmoja wao akanyanyuka kwenda
kumfatwa Agnes kwenye eneo la kuuzi vinywaji ili kuzungumza ombi la bosi
wake analo lihitaji
ENDELEA
“Habari yako dada?”
Kijana
wa Muntar alimsalima Agnes ambaya kwa haraka akaliachia tabasamu lake
mdomoni na kuufanya uso wake kuzidi kunawiri kwa uzuri
“Salama mamo vipi?” Agnes alizungumza kwa sauti nyororo ya kuvutia hadi muhudumu kiume wa vinywaji akaguna
“Salama.....kwa jina mimi ninaitwa Kibopa na yule pale alavalia cheni nyingi ni bosi wangu anaitwa Muntari”
“Aahaa nashukuru kuwafahamu,Samahani kaka ninaomba unipatie Red’s mbili za baridi kiasi”
“Muhudumu mpe katon nzima pesa nitalipa mimi?”
“Jamani kaka yangu mimi sio mnywaji sana”
“Ahaa usijali nyingine unaweza kunywa leo au hata kesho”
“Asante sana”
Muhudumu akamkabidhi Agnes katoni ya kinywaji alicho muagizia na kibopa akatoa pesa na kumlipia muhudumu.
“Sasa sister kama huto jali ninaomba namba yako ya simu”
Agnes bila wasiwasi akamtajia Kibopa namba yake ya simu,wakaagana ana Agnes akarudi sehemu alipo Rahab
“Jamaa ameshaingia mkenge sasa kazi ni moja sawa”
“Hapo ndipo ninakupendea Ag”
“Chezea mimi wewe,kumbe mtu ukiwa na kalio kubwa nalo linasaidia”
Wakacheka
na kufungua vinywaji na kuanza kunywa taratibu.Muntar akakabidhiwa
namba na Kibopa na akaipiga na Agenes akaipokea na kama kawaida na sauti
yake nyororo aliyobarikiwa kutoka mbinguni akazungumza
“Nani mwenzangu?”
“Ukigeuka upande wako wa kushoto utaniona nimevaa shati jeupe na cheni za dhahabu”
Agnes akageuka na kumfanya Muntar kupunga mkono akimuashiria kuwa ni yeye ndiye aliye mpigia simu
“Mrembo nakuomba basi uje kujumuika name hapa?”
“Naona aibu labda nije na mwezangu”
“Hilo tuu hakuna tatizo ni wewe tuu”
“Sawa ninakuja”
Agnes
akakata simu na kumtazama Rahab kwa pamoja wakatabasamu na wakasimama
na kuanza kutembea kwa mwendo wa maringo na kupishwaviti na wapambe wa
Muntar kisha wakakaa
***
Dokta
Wiliama akawashusha kwenye gari Anna,Halima na Fety mbali kidogo na
hotel ya Serena huku kila mmoja simu yake ikiwa na salio la kutosha
pamoja na picha ya Karim Yussuf kijana mwenye umri mdogo ila anasifika
sana kuwa na utajiri mkubwa kutokana na Sheli za mafuta anazo zimiliki
kila kona ya mikoa ya Tanzania.Kila mmoja akaingia Hotelini kwa muda
wake na kuelekea kuketi katika upande wake ila kwa pamoja wakawa na
mawasiliano ya ujumbe mfupi wa meseji.Kutokana ni muda wa jioni hawakuwa
na papara kwani watu wengi bado hawakuwa wameingia Hotelini kuendelea
na starehe zao.Macho ya Fety yakatua kwa jamaa anayeingia kwenye mlango
wa kuingilia akiwa ameongozana na mwanamke mrembo
{Nimemuona}
Fety
akausamba ujumbe kwa wezake ambao wapo maeneo ya tofauti kwenye hoteli
na taratibu simu yake akaichomeka kwenye suruali yake na kuendelea
kumtazama Karim ambaye moja kwa moja aka anaelekea sehemu yenye milango
ya lifti zinazo kwenda juu na kushuka chini,Kutokan-a na Lifti kutumika
ikamlazimu Karimu na mpenzi wake kusimama kwa muda kuzisubiria.
Kwa
haraka Fety akasimama na kupiga hatua za haraka kabla hajafika sehemu
alipo Karimu,lifti ambayo wanaisubiria ikafunguaka,Karim na mpenzi wake
wakingia ila kabla haijajifunga Fety akawahi kuizuia na kuingia
“Habari zenu?”
“Salma”
Karimu
kutokana na kutokuwa na aibu akaanza kumshika shika mpenzi wake na
kuchezeana katika sehemu zao nyeti.Mcho ya Fety yakawangalia kwa umakini
kisha akayahamishia masho yake kwenye kamera mbili za ulinzi zilizopo
ndani ya lifti kabla hajafanya kitu chochote akastukia lifti ikisimama
hii ni baada ya mpenzi wa Karimu kuminya kitufe cha kuisimamisha lifti.
Kufuma
na kufumbua Fety akastukia ngumi kutoka kwa mpenzi wa Karim ikitua
kwenye shavu lake na kumsfanya kuweweseka kasha akaanza kuikwepa mikono
inayoimjia mwilini mwake kutoka kwa Karimu na mpenzi wake Shamsa mwenye
asili ya kiarabu.

Post a Comment