Polisi akikamata haulizi itikadi ya mtu - Mwigulu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu
Nchemba amesema Jeshi la Polisi nchini linafanya kazi kwa mujibu wa
sheria na taratibu na linapomkamata mtu halimuulizi itikadi ya chama
chake.
Waziri Mwigulu
ameyasema hayo leo bungeni Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa
Viti Maalumu (CHADEMA) kutoka Mwanza Susan Masele aliyetaka kupata kauli
ya serikali juu ya askari polisi ambao wanawabambikizia kesi wafuasi wa
UKAWA kwa kuwapa kesi za uchochezi.
“Jeshi
la polisi linapowakamata watu, haliwaulizi itikadi zao, na
linapowafikisha mahakamani haliwaulizi kadi za vyama vyao bali huangalia
kosa ambalo limefanyika” Amesema Waziri Mwigulu.
Aidha
waziri amesema kuwa wananchi wanaweza kupeleka malalamiko yao kuhusu
Jeshi la Polisi katika vyombo vinavyoshughulikia sheria au katika makao
makuu ya jeshi kwa kuwa kuna kitengo kinachoshuhulikia malalamiko ya
wananchi.
Sambamba na hayo Waziri Mwigulu
ameweka bayana kwamba askari ambao hukutwa na mashtaka ya
kuwabambikizia wananchi kesi au mambo mengine na yakibainika kuwa ni ya
kweli huadhibiwa na kulingana na sheria.

Post a Comment