MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUNUNUA COMPUTER
Asante kwa kutembelea blog yangu(www.mtegachemit.blogspot.com). asante kwa kuungana nami kwenye darasa
la leo. hili swali limeoulizwa na mmoja wa wafatiliaji wa masomo yangu
kwamba akitaka kununua computer aangalie vitu gani? kiukweli kuna vitu
vingi sana vya kuangalia kabla hujanunua computer(iwe desktop au laptop)
iwe mpya au ya zamani. leo nitaongelea mambo makuu matatu ambayo ni
muhimu sana kuyazingatia kabla hujanunua computer. yafuatayo ni mambo
muhimu sana ya kuzingatia.
1. UKUBWA LA RAM
neno ram ni kifup cha neno RANDOM ACCESS MEMORY. kazi kubwa ya RAM ni
kuisaidia computer kufungua mafile na mafolder mbalimbali, pia hufihadhi
taarifa kwa muda mfupi na taarifa hizi huwa zinafutika pale tu
unapozima computer na kuwasha. ili computer iwe faster au iwe slow
hutegemea sana ukubwa wa RAM. ndio maana RAM isipokuwepo kwenye computer
yako haiwezi kuwaka, itaishia kuonesha charge inaingia lakini haiwaki.
kwahiyo unapotaka kununua computer hakikisha RAM inakuwa na ukubwa wa
atleast 2GB
2. UKUBWA WA PROCESSOR
Processor ni kama ubongo wa computer yako, kitu chochote kinachofanyika
kwenye computer processor ndio hufanya kazi hiyo. yan mfano unabonyeza
herufi M na inatokea, kitendo hiki cha kubonyeza na kutokea huwa
kinafanywa na PROCESSOR. kwa jina lingine processor huitwA CENTRAL
PROCESSING UNIT. kwahiyo unapotaka kununua computer ni muhimu
kuhakikisha processor yako inaukubwa kias, atleast kuanzia 2Ghz
3. UKUBWA WA HARD DISK
hard diski ndio memory ya computer yako. humo ndio huhifadhiwa vitu
vyote unavyoviweka kkwenye computer, mfano unapoweka mizki au movies au
mafile yako yote huhifadhiwa kwenye HARD DISK, kwa kifupi huwa inaitwa
HDD. ukubwa wa HDD HUTEGEMEANA NA MATUMIZI YA COMPUTER HUSIKA. kama unamatumizi makubwa nunua computer yenye HDD kubwa. na kinyme chake ni sahihi.NB
yapo mambo mengi ya kuzingatia kabla hujanunua computer hayo niliyoelezea ndio muhim zaid na nirahisi kuyatambua, pia kama ni laptop ni vema ukajua charge inakaa masaa mangapi kabla hujaiununua.
ninaamini somo hili litakuwa msaada kwako ulieuliza pia kwa wasomaji wengine kwani wengi wamekuwa na tatzo kama hili asante.
ASANTE SANA
kwa msaada :0758297744

Post a Comment