(KUMBUKUMBU ZA KWELI ZA MAISHA YANGU)-ERICK SHIGONGO
(KUMBUKUMBU ZA KWELI ZA MAISHA YANGU)
SITAKI kuyafanya maisha yangu yawe siri, nataka watu wote wanifahamu. Ndiyo maana nimeamua kuandika kumbukumbu zangu hiki ili kuelezea yale ninayoyakumbuka maishani mwangu, tangu nilipozaliwa mpaka siku nitakapokoma kuandika.
Ninaamini yatakuwapo mengi ya kujifunza, kutia moyo na pengine kumwonya mtu mwingine asiyafanye kwani nimefanya makosa mengi sana maishani mwangu. Mengine ni ya aibu lakini nitayasema hadharani na ninapotakiwa kuomba msamaha nitafanya hivyo.
Nawakaribisha kwenye kumbukumbu zangu za maisha ambazo nimezitunza kwa muda mrefu, kwa lengo la kuandika kitabu. Najua yatakuwapo ya kuchekesha, kutoa machozi na kuinua mioyo ya waliokata tamaa.
****
NINA umri wa miaka mitano, ni asubuhi ya siku na mwezi nisioukumbuka mwaka 1976. Kuna ukungu kila mahali, umande umetapakaa kwenye nyasi. Baba yangu amenishika mkono ananipeleka Kijiji cha Ishigwandama kilichokuwa kama kilomita mbili kutoka kijijini kwetu Mwangika.
Ingawa natetemeka kwa baridi kali na meno yakigongana, kwani sina sweta mwilini mwangu na manyunyu ya mvua yanadondoka, bado moyo wangu una furaha kwa sababu ni siku ya kwanza napelekwa shuleni kuanza darasa la kwanza kwenye shule ya TAPA yaani kifupi cha ‘Tanganyika Parents Association’, ilivyokuwa inajulikana Jumuia ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati huo.
Tunatembea kidogo, ninachoka, baba anaamua kunibeba begani. Ni mzee maskini, hakusoma hata darasa moja lakini anapenda elimu na anaamini ndiyo itakayosaidia watoto wake maishani.
“Ng’wanone, yaya iligusha, ukasome getegete! Uligwa?” anasema baba yangu kwa lugha ya Kisukuma tulipokaribia shuleni, akimaanisha “Mwanangu, usiendekeze michezo shuleni, usome kwelikweli, unasikia?”
“Nali…gwa!” (Nasi…kia) naitikia huku meno yakigongana.
Shuleni ananishusha mabegani mwake na kuanza kutembea. Kinachoonekana mbele yangu ni majengo madogomadogo ya nyasi. Ni kama mabanda ya kuku, nje kuna watoto wengi, wote wakiwa hawana viatu kama nilivyo mimi. Baadhi yao hawana hata mashati, pamoja na baridi hiyo wapo kifua wazi.
Wamepauka kama vile hawakuoga jana yake huku wengine wakiwa na vipande vya chakula mikononi. Nilipoangalia vizuri nikagundua ni kiporo cha ugali.
Namwona mtoto mmoja jirani yetu ambaye huwa nacheza naye siku zote. Najichomoa kwenye mkono wa baba na kumkimbilia. Tunasimama pamoja tukiwa na furaha, ni siku ya kwanza shuleni. Huyu anaitwa Joki (hivi sasa ni marehemu, alifariki miaka michache iliyopita wakati naandika kitabu hiki).
Haukupita muda mrefu sana akaja mtoto mwingine, pia namfahamu, anaitwa Malila (yupo kijijini mpaka leo, ni rafiki yangu mkubwa).
Muda mfupi baadaye mwalimu anajitokeza, simkumbuki jina na tunamsalimia kwa Kisukuma lakini anakataa na kututaka tuseme maneno “Shikamoo Mwalimu”. Ni maneno mageni kwang
u kwani sijazoea kuyatumia nyumbani.
Kwangu ni kama maneno yaa Kichina, hivyo nalazimika kuyazoea kwani ndiyo yatakayokuwa yakitumika shuleni kila siku.
Furaha niliyonayo moyoni haina kipimo kwani nilitamani sana kusoma na siku zote nilipowaona watoto wakipita nyumbani kwetu wakielekea shuleni moyo uliniuma. Hakika siku hii ya leo niliisubiri kwa muda mrefu.
“Sasa tutawapima, waliotimiza umri tu ndiyo watakaoanza shule!” Ilikuwa ni sauti ya mwalimu baada ya salamu. Moyo wangu ukashtuka kugundua kuwa kumbe kuna watu wasingeanza darasa la kwanza kwa sababu ya umri wao.
Wote tukapangwa kwenye mstari mrefu na mwalimu akawa anapita na kumwambia mwanafunzi mmojammoja anyanyue mkono wake wa kuume na kuupitisha juu ya kichwa na kugusa sikio la upande wa kushoto. Waliogusa waliwekwa upande mmoja na ambao hawakugusa waliwekwa upande wa pili.
“Wewe mtoto wa James, acha ujanja! Weka mkono wako vizuri, weka katikati ya kichwa usiweke kichogoni!” mwalimu alisema kwani mkono wangu ulikuwa haugusi sikio. Ili kulifikia, ilibidi niusogeze kwa nyuma ndipo nikafanikiwa kuligusa.
Nikajaribu weeee! Lakini sikuweza. Bila huruma, mwalimu akanisukumizia upande wa watu ambao walishindwa kugusa sikio. “Hawa warudi nyumbani mpaka mwaka kesho, wakue kidogo.”
Haikuwa shule tena, iligeuka kuwa hospitali au kliniki kwani mimi ndiye niliyeongoza vilio vya wanafunzi wote waliokataliwa kuingia darasa la kwanza. Nikagalagala chini huku nikimwita baba ambaye alifika na kuninyanyua.
Akaanza kunibembeleza ninyamaze huku akiniambia nivumilie tu mwaka kesho haukuwa mbali. Sikukubali, niliendelea kulia kwa nguvu nikiamini mwalimu angebadilisha mawazo lakini haikusaidia. Wenzangu wakaingia darasani nami nikabebwa na baba begani na kuanza kurejea nyumbani.
Njia nzima nililia, nilifika nyumbani macho yakiwa mekundu na yakiwa yamevimba na sauti ikawa imepotea. Inawezekana kabisa nilikuwa ninafanya hivyo kwa kudeka.
“Nyamaza mwanangu utasoma tu!” ilikuwa ni sauti ya mama yangu.
“Labda jaribu wewe, mimi nimeshindwa, mtoto hasikii!” baba aliitikia.
Kubembelezwa na mama kulininyamazisha. Baada ya muda mfupi, nikasahau na kuendelea na michezo. Kumbukumbu ilinirejea nilipowaona baadaye Joki na Malila wakirejea kutoka shuleni. Roho iliniuma mno lakini nikajipa moyo na kuamini mwaka kesho na mimi ningeanza shule ingawa wao wangekuwa tayari darasa la pili.
Unajua nini kiliendelea?
Tukutane Jumamosi mahali hapa.
Usikose kushare kwa ajili ya marafiki zako.
Unaweza kunipata Instagram kwa ericshigongo

Post a Comment