ATHARI TATU(3) ZA KUJIKWEZA KUTOKANA NA MAFANIKIO ULIYOYAPATA
Habari za wakati huu
ndugu msomaji wa makala za mtandao huu(www.mtegachemit.blogspot.com) ni matumaini yangu
kuwa hu mzima na unaendelea vyema katika kupambana ili tu kuweza kujiletea
mafanikio, nami nakusihi endelea kupambana bila kuchoka maana mafanikio ni
mapambano ambayo yanakuhitaji kuwa imara zaidi na zaidi. Karibu leo tujifunze
kwa pamoja juu ya tabia moja ya kuiepuka pindi upatapo mafanikio.
Kila mtu kwa namna yake
na kwa aina yake amekuwa akitafuta mafanikio na kuyapata, lakini sina uhakika
kama katika wapambanaji hawa wanao pambana ili kuyapata mafanikio kuna anayetaka
mafanikio ya muda mfupi kutokana na sababu hii ndio maana nakusihi sasa kuwa
usijikweze kutokana na mafanikio uliyoyapata, maana wapo watu ambao pindi
wapatapo mafanikio hujikweza na kujifanya kuwa wao ni mungu watu yaani wanajua
kila kitu hawaambiliki, hawashauriki wala kufundishika kwa namna yoyote haswa
na watu ambao wako chini yao kiuwezo. Zifuatazo ni athari za kujikweza na
madhara yake
Kumbuka biblia inasema
“ajikwezae atashushwa”, sio jambo la busara kwako wewe eti kisa una mafanikio
basi ndio ukajiona bora sana kuliko watu wengine maana jambo hili linaweza
kupelekea ukawa na dharau sana kwa
watu wa chini yako na swala hili kama wewe ni mkuu/bosi wa kampuni fulani
linaweza kuathiri sana utendaji wa kazi wa wafanyakazi wako na hatimae kampuni
yako ikaja kufilisika maana hakuna mfanyakazi ambae anapenda kufanya kazi
katika mazingira ambayo anadharaulika na dharau kwa wafanyakazi huwa inashusha
morali yao ya kufanya kazi hivyo ni rahisi kwao wao kuanza kufanya kazi ovyo
ovyo na hatimae kampuni ikakosa maendeleo kwa kiasi kikubwa.
Kujikweza hukufanya ushindwe kushaurika, kwa kuwa wewe
unajikweza na kujiona kuwa wewe ndio wewe basi hata kama unashauriwa jambo zuri
wewe utapuuzia maana unajiona wewe ndio wewe hivyo kusikiliza ushauri kwako
inakuwa ngumu. Kutokusikiliza ushauri wa watu sio jambo la busara maana unaweza
kupuuzia ushauri hata wenye tija, na kupuuzia huku hutokana na sababu kuwa wewe
ushajikweza, yaani kama wewe ni bosi basi unaona kuwa mfanyakazi hawezi kutoa
ushauri wowote wenye kunufaisha kampuni au shirika lako, jambo ambalo ni kupotoka
maana kampuni bora na zinazofanya vizuri hapa duniani ni zile ambazo bosi
anashirikiana vyema na wafanyakazi wake kwa kila jambo haswa bosi kusikiliza
ushauri wa watu wa chini yake maana wao ndio wafanyakazi, kama ni bidhaa wao
ndio watengenezaji, wao ndio wasambazaji na wauzaji hivyo wakikushauri kuhusu
bei ya bidhaa mfano ni muhimu ukawasikiliza maana wewe upo kama msimamizi
ambapo mambo mengi utakuwa huyajui kiuhalisia ila kupitia wao unaweza kuyajua.
Kujikweza kutakufanya usiwe msikilizaji bali uwe mzungumzaji tu,
jambo jingine ambalo linaweza kuhatarisha mafanikio yako kutokana na kujikweza
kwako ni kuwa , kutokana na kujikweza kwako basi wewe utabaki kuwa mzungumzaji
kuliko msikilizaji jambo ambalo ni hatari sana katika maisha. Maishani watu
wanaofanikiwa ni wale ambao wana uwezo mkubwa wa kusikiliza watu pindi
wanapozungumza na sio wao wanataka kusikilizwa muda wote. Mtu anayependa
kuzungumza muda wote kuliko kuwasikiliza wenzake anakuwa amejikweza na kujiona
kuwa yeye ni bora kuliko sasa kama hupendi kuwasikiliza wenzako basi na wao ipo
siku watachoka kukusikiliza vile vile na hapo ndipo utakapo pata anguko lako na
kubaki kuyasikia mafanikio.
Nimekuwekea athari tatu
muhimu ambazo zinaweza kukupata kutokana na kujikweza kwako hivyo hata kama una
mafanikio kiasi gani hakikisha kuwa hujikwezi maana kujikweza huleta anguko na
ukianguka katika mafanikio kuinuka huwa ni kazi ngumu sana.
Post a Comment