Header Ads

Vitu 3 ambavyo Manji hakutendewa haki katika mkutano alipoomba kuikodi Yanga.


Kwa sasa headlines zinazotawala katika vichwa vya habari vya mitandao na magazeti ya michezo ya Tanzania ni kuhusiana na bilionea Mohammed Dewji kuomba kuinunuaSimba na mfanyabiashara na mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji kuomba wanachama wamkodishiea Yanga kwa miaka 10.
Manji ameomba akodishiwe Yanga kwa miaka 10 yaani apewe timu na nembo ya klabu lakini mali na majengo mengine yabaki mali ya klabu kama kawaida, katika kuikodisha Yanga, Manji ameahaidi klabu kupata faida ya asilimia 25 na yeye asilimia 75 na kama ikitokea hasara yeye ndio itakula kwake na sio klabu.
Kitendo cha Manji kuomba kuikodi Yanga kimekuwa kikiandikwa kwa kiasi kikubwa na kujadiliwa katika mitandao ya kijamii kama suala geni, lakini kwa mujibu wa maelezo yake anasema ni jambo ambalo lipo katika katiba ya Yanga ya mwaka 2006.
Wanachama wa Yanga waliohudhuria katika mkutano mkuu August 6 2016 Diamond Jubilee hawakumtendea haki Manji, kwa kutomuuliza mambo matatu kuhusu hoja yake.
*Manji alitakiwa aulizwe kwa nini apewe asilimia 75 na sio 25? swali ambalo halikuwepo 
*Kwa nini akodishiwe kwa miaka 10 na sio miwili au mitatu?
*Utaratibu gani anataka kuutumia kukodi kama ni fedha angetoa kiasi gani?

No comments

Contact us:Email:godfreymtega@gmail.com/WhatsApp-+255758297744/+255716824009 . Powered by Blogger.