Header Ads

VIDEO: Manji alivyowaomba wanachama wamkodishie Yanga na nembo kwa miaka 10.


Mfanyabiashara na mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji katika mkutano mkuu na wanachama wa Yanga uliofanyika August 6 katika ukumbi wa Diamond Jubileeameomba wanachama wamkodishie timu ya Yanga na nembo ya klabu kwa kipindi cha miaka 10.
Manji ameomba wanachama wamkodishie timu na nembo ya klabu hiyo kwa kigezo kuwa timu imekuwa ikijiendesha kwa hasara na kuwa mwaka unaokuja itashindwa kuepuka hasara ya bilioni 1.9, hivyo anaomba akodishiwe timu na mali za klabu ziendelee kuwa chini ya klabu kama kawaida.
“Hiki kitu kipo kwenye rasimu na katiba yetu ina ruhusu, naomba nipangishiwe timu na nembo kwa kipindi cha miaka 10, majengo na mali za klabu ziendelee kuwa za klabu mimi nahitaji timu na nembo, ikipatikana hasara ya kwangu faida klabu itapata asilimia 25 na 75 za kwangu, klabu hii haina nguvu ya kubeba hasara ya bilioni 1.9 ya mwaka ujao”

video--------https://youtu.be/dCAoUP58jAM

No comments

Contact us:Email:godfreymtega@gmail.com/WhatsApp-+255758297744/+255716824009 . Powered by Blogger.