PICHA: Simba imeiadhibu AFC Leopard, Mavugo akithibitisha ubora wake.
Jumatatu ya August 8 2016 klabu ya wekundu wa Mzimbazi Simba ilihitimisha kilele cha wiki ya Simba sambamba na maadhimisho ya miaka 80 ya klabu hiyo kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya AFC Leopard ya Kenya uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Katika mchezo huo ambao Simba walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 4-0, kochaJoseph Omog aliwatumia wachezaji wake nyota wa kimataifa kama sehemu ya kuwatambulisha, mashabiki wa Simba ambao walikuwa Taifa walikuwa wakimsubiri kwa hamu mshambuliaji wao mpya kutoka Burundi Laudit Mavugo aliyeingia kipindi cha pili.
Simba ambao walionekana kuielemea AFC Leopard kipindi cha pili na kuwafunga magoli yote manne, Ibrahim Ajib alifanikiwa kufunga goli dakika ya 38 na 60 na baadae Shiza Kichuya alipachika goli la tatu dakika ya 66 baada ya kupokea assist safi kutoka Laudit Mavugo ambaye pia alihitimisha ushindi wa Simba kwa kupachika goli la nne dakika ya 84.
ALL GOALS: SIMBA VS COASTAL UNION FA CUP APRIL 11 2016, FULL TIME 1-2
https://youtu.be/4ZD1VPjVyGA
ALL GOALS: SIMBA VS COASTAL UNION FA CUP APRIL 11 2016, FULL TIME 1-2
https://youtu.be/4ZD1VPjVyGA
Post a Comment