Header Ads

PICHA: Azam FC wameiadhibu Yanga kwa mikwaju ya penati na kutwaa Ngao ya Hisani

August 17 2016 kuelekea kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu soka Tanzania bara uwanja wa Taifa Dar es Salaam ulichezwa mchezo wa Ngao ya Hisani kati ya Mabingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2015/2016 klabu ya Dar es Salaam Young Africans na mshindi wa pili wa Ligi Kuu Azam FC hiyo ikiwa ishara ya kukaribia kuanza kwa msimu mpya wa Ligi.
IMG_0306
Katika mchezo huo ambao dakika 45 za kwanza zilikuwa zinaonesha kuna kila dalili zaYanga kuondoka na Ubingwa wa Ngao ya Hisani, umemalizika kwa Azam FC kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penati 4-1, hiyo inatokana na mchezo huo kumalizika kwa sare ya goli 2-2. Hii ni mara ya nne mfululizo Yanga na Azam FC wanacheza mchezo wa Ngao ya Hisani, huku Yanga akiwa amechukua mara tatu katika misimu mitano na Azam FC mara mbili.
IMG_0323
Kipindi cha kwanza kilikuwa kizuri kwa Yanga baada ya dakika ya 20 Donald Ngomakupachika goli la kwanza kwa mkwaju wa penati na dakika 2 baadae kuongeza goli la pili kwa kutumia vyema pasi ya Amissi Tambwe, kipindi cha pili ndio Yanga waliendelea kumiliki mpira na kila mtu akiamini mchezo utamalizika hivyo.
IMG_0289
Dakika ya 74 Azam FC walipata goli kupitia kwa Shomari Kapombe lakini kujisahau kwaYanga walijikuta wakisababisha penati na John Bocco akaisawazishia Azam FC katika dakika za nyongeza, kwa upande wa mikwaju ya penati za Azam FC zilipigwa na John BoccoShomari KapombeHimid Mao na Kipre Bolou wakati penati za Yangazilipigwa na Deogratus Munish huku Haruna Niyonzima na Hassan Kessy walikosa.
IMG_0349

No comments

Contact us:Email:godfreymtega@gmail.com/WhatsApp-+255758297744/+255716824009 . Powered by Blogger.