MBINU SITA(6) RAHISI ZITAKAZOWEZA KUKUSAIDIA KUTAMBUA KIPAJI CHAKO,NA JINSI UTAKAVYOWEZA KUKITUMIA
Fahamu kuwa Mtu mwenye kipaji kisichoendelezwa kwa kupewa fursa ya kukifanyia kazi hana uwezo wa kukitambua. Hali hii ndiyo iko kwa watu wengi duniani. Ya kuwa wana vipaji ambavyo havikuwahi kupewa fursa ya kufanyiwa kazi ili vijidhihirishe. Kwa sababu hiyo hujikuta wakitumika kupitia vipaji vya watu wengine .Namna hii huwafanya kukosa hamasa ya kufanya zaidi na hivyo kila kitu kwao huwa kigumu au hakiwezekani isipokuwa kwa wenye vipaji halisi.
Tambua kuwa kipaji sio ndoto kama tulivyozoea kufikiri. Bali ndoto inatakiwa ije baada ya kutambua kipaji. Mara nyingi tumezoea kuwauliza watoto wadogo watueleze ndoto zao na kuchukulia kuwa hivyo ndiyo vipaji vyao. Hapo tunakuwa hatuko sahihi hata kidogo. Mtu yeyote anaweza kuwa na ndoto ya kitu chochote au ya kuwa mtu yeyote lakini si kipaji. Fahamu kuwa kipaji hakiwezi kuja kwa kukitamani tu. Kwa sababu ni kitu ambacho kipo ndani yetu tangu tunazaliwa kila mmoja kwa namna yake. Kipaji hujijenga chenyewe ndani ya binadamu bila kukijengea picha yeyote. Ni uwezo wa kiasili wa kuzaliwa nao na sio wa kuhamasishwa. Hautokani na mambo yaliyokwisha kuwapo bali ni uwezo wa kipekee sana anaokuwa nao binadamu aidha katika kutenda, kufikiri au kusema. Kila mtu anatofautiana na mwenzake kwa uwazi kabisa hata kama wako katika kundi la kipaji cha aina moja.
Tambua kwamba akili ya binadamu ina uwezo wa kufanya kila kitu kwa sehemu. lakini haina uwezo wa kufanya kwa ufanisi mkubwa kama ambavyo inatokea kwa mtu mwenye kipaji. Tusijidanganye kwa kung’ang’ania vitu ambavyo sio sehemu ya vipaji vyetu na badala yake tuweke mkazo kwa vinavyoendana na vipaji tulivyonavyo. Zifutazo Ni Mbinu sita (6) rahisi zitakazoweza kukusaidia kutambua kipaji chako, Na jinsi unavyoweza Kukitumia.
Mbinu sita (6) rahisi zitakazoweza kukusaidia kutambua kipaji chako, Na jinsi unavyoweza Kukitumia.
1. Swali muhimu la kujiuliza.
Wazazi au walimu wako wameshawahi kugundua uwezo wako wa jumla katika kipaji cha jumla mfano taaluma, michezo, kuzungumza, nk? Ulishawahi kujulishwa au kupata tetesi? mpaka sasa kipaji hicho kimeshajitokeza na kukufanya uwe na mahala pamoja unapofanya vizuri zaidi ? kama ndiyo tumia fursa hiyo kipaji kitatokeza.
2. Chunguza mazingira yako.
Angalia mazingira ya unachofanya kama yalitokana na uwezo wako wa asili au ulijiingiza kwa kuhamasishwa na mtu, shida, au tamaa ya kutajirika haraka. Tafuta kile kinachotokana na uwezo wako wa asili ili kipaji chako kiweze kufanya kazi.
3. Angalia ulichokuwa unakifanya.
Angalia kama kuna ulichokuwa ukikifanya hapo zamani ambacho hata kama hukukifanya kwa ufanisi kwa kukosa maarifa lakini kilikupa upekee .Lakini kiwe kilitokana na uwezo wako wa asili na ulifanya mara kwa mara. Kiendeleze na baada ya muda kitakupa mwelekeo wa wapi uende na hivyo kufanya uwe tofauti na wengine.
4. Angalia unachokifanya sasa.
Angalia kama unavyovifanya sasa hata bila kutumia maarifa mengi kimojawapo unakifanya kwa ufanisi mkubwa kuliko vingine vyote na kwa upekee. Hicho unachokifanya vyema zaidi ndicho kipaji chako usikidharau ukikikuza kila mtu atakiheshimu. Hata huheshimika ya nyumba ni baada ya kumalizika ujenzi, katika msingi mtu yeyote anaweza hata akajisaidia haja ndogo.
5. Nini kilikutambulisha na kinachokutambulisha.
Angalia katika unavyovifanya au ulivyovifanya ni kipi kilikutambulisha au kinakutambulisha na kukufanya ukubalike kipekee na sio kutokana na kiwango chako cha kisomo. Kipaji halisi hakitegemei kiwango cha kisomo, bali uwezo wa asili ndio hutawala katika kutenda jambo. Katika kiwango chochote cha elimu bado uwezo wa asili utachukua nafasi na kutawala katika utendaji na kukufanya wewe ndiyo upate sifa na sio elimu yako.
6. Ni nani aliyekwambia una Kipaji?
Jiulize kama umeshawahi kuambiwa una kipaji? Je ni kipaji gani? Umeshawahi kuambiwa mahala kwingine na hapo maneno kama hayo? Hicho ndicho unachokifanya mara kwa mara kwa ufanisi kuliko mengine?.
7. Tazama hisia zako.
Angalia kama unachofanya unahisia nacho au unafanya kwa sababu hauna kazi nyingine? Na hisia zako za ndani zinasemaje? Jali zaidi hisia zako za ndani sana zinazo husiana na uwezo wako bila kujali vitisho kwa sababu kipaji kina nguvu kuliko kitisho chochote kilichoko mbele yako. Kama wewe hujawahi kuhisi au kusikia chochote kuhusu kipaji chako basi ni kwa sababu ya kukosa nafasi ya kukionyesha. Fanya kila unachohisi kinatokana na uwezo wako wa asili hata kama kimewahi kufanywa na mtu mwingine. Asante kwa kusoma makala hii ,Tunakutakia kila la kheri katika safari ya kutambua kipaji chako na kuweza kukitumia ili kuweza kufikia mafanikio makubwa, Daima tutaendelea kuwa pamoja mpaka maisha yetu yaimarike. TUKO PAMOJA.


Post a Comment